Wananchi Arusha wanaunga mkono hatua ya Rais Magufuli kutumbua majipu hadharani

TUNDE

Senior Member
Apr 23, 2016
129
77
Anachokifanya Mheshimiwa Rais ni kitendo cha kiunguana kabisa wanasema wananchi wa Arusha. Rais akitumbua jipu haina maana kwamba mtuhumiwa ameshafukuzwa kazi, ila mtuhumiwa atapisha uchunguzi na kama uchunguzi utabaini kwamba mtuhumiwa hakuwa jipu basi mhusika ni mfanyakazi safi na atarudishwa kazini kama kawaida.

Kwa njia hiyo hakuna mahali popote watuhumiwa majipu wanaonewa au wataonewa. Kama alivyosema Mhe Rais mwenyewe kwamba yeye ndiye aliyeteua hao anao wawajibisha. Mhe Rais alisema wakati anateua wahusika hakufanya kificho, aliutangazia umma kwamba kamteua Fulani kushika wadhifa fulani.

Rais habanwi na sheria kwamba akitaka kutengua nafasi ya mtu aliyempa madaraka fulani atumie njia gani. Kwa hekima ya Mhe Rais, ameona atumie njia ileile aliyotumia wakati anampa fulani huyo madaraka hayo.

Utafiti niliofanya, unaonesha kwamba katika wananchi 100 walioulizwa ikiwa hatua ya Rais kutangaza kutumbua majipu hadharani wanakubaliana nayo au la, 80 walionesha kukubaliana na hatua ya Mhe Rais kutumbua majipu hadharani. Kwa maana nyingine ni kwamba, katika kila wananchi 100, 80 wanamtaka atangaze hadharani majipu yanayotumbuliwa.

Hivyo, 80% ya watanzania waliohojiwa walienda mbali na kusema kwamba nia ya Rais kutumbua majipu hadharani ni kutoa fundisho kwa wengine wasifanye vitendo vya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Wananchi wengine wamesema, pamoja na kwamba kutumbuliwa huko kunatokana na tuhuma ambazo hazijathibitika, lakini kwa kiwango kikubwa tuhuma husika zinakuwa zimeshachunguzwa na kuacha kiasi kidogo sana cha shaka. Kiasi hicho cha shaka ndicho Mhe Rais ameachia mamlaka nyingine kujiridhisha kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Wengine wakasema majipu yote yaliyotumbuliwa tayari wana hatia kikazi na anachokitaka Rais ni kupelekwa mahakamani na hatimaye kufunguliwa mashitaka hatimaye wafungwe jela.

Wakati hayo yakiendelea, sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha wanaunga Mkono jitihada za Mheshimiwa Rais katika kutaka kuleta heshima ya Mtumishi wa umma. “Watumishi wa umma na hasa waliopewa dhamana ya kuongoza ni lazima waoneshe njia na wasiwe sehemu ya kukwamisha maendeleo ya taifa kama inavyoonekana sasa” alisema mtumishi mmoja. Mwingine alisema, vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka vimekuwa kama kawaida katika chuo hiki.

Kila siku utasikia vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Zaidi ya Tsh 3.2 Bilioni zimeshaliwa kifisadi katika kipindi cha kati ya 2011 mpaka 2015. Hapo hujahesabu mishahara hewa, Mkuu wa Chuo na wasaidizi wake wawili kujiongezea mshahara, Ajira za upendeleo, Kunyanyasa wafanyakazi, Wanafunzi wenye umri mdogo kupata ujauzito kiholela wakiwa chuoni na upendeleo wa wazi kwa baadhi ya wafanyakazi nk.

Wafanyakazi hao wanasema ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kuchukua hatua zinazostahili, kwa kufika chuoni na kutumbua wahusika wote hadharani, kwasababu vitendo vinavyofanywa na Menejimenti ya Chuo si kificho na imeonekana mchana kweupe ikihaha kila kukicha namna ya kuficha ukweli huo lakini haiwezekani. Katika harakati za kuficha ukweli huu, huenda Bw. Gasto Leseiyo (Afisa Habari wa Chuo) akaagizwa kukanusha habari hii kupitia gazeti la Mwananchi Kesho ameeleza mfanyakazi mmoja.

Mungu Mbariki Rais Magufuli, Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom