Blaki Womani
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 11,228
- 13,450
I see ....nitakuja baadae nina maswali kibao kwa hawa wanandoa
Kazi kweli kweli,
Kama hiyo ndoa ina mawasiliano mazuri hiyo kitu ilitakiwa kuwa na taarifa mapema kuhusu huyo mgeni na safari ya kutalii.
Hilo dume nalo noma kweli anachukulia hiyo kitu kidogo but assume naye mke akaja na classmate wake mwanaume ....then safari ya ngorongoro siku mbili. Atajisikiaje?
Mshauri huyo dada waongea fresh na mume kutegemeana maisha yao wanayoishi. Na kama kosa moja wasameheana maisha mazuri yaendelee.
Mpe pole. Maana yake nimepiga picha ndio mke wangu nafanyia hivyo..noma dhamira ingenisuta sana.
awe na imani na mumewe! Kwan kuna nn kmemfanya ahisi co rafk ya mumewe na ni nymba ndgo? Wkt mwngne wadada2nakarbsha stress wnyewe! Aamin alchoambiwa.
Katika ndoa yoyote ile ukiona mume hatoi ushirikiano kwa mkewe kama kumpa taarifa za nini kinachoendelea katika maisha yao ujue hapo kuna tatizo.Jana usiku amekuja rafiki yangu ameolewa na ana watoto 2 wiki mbili zilizopita mumewe alikuja na mgeni mwanamke nyumbani bila taarifa kwa mkewe akamtambulisha ni mwanafunzi walisoma nae wakati akiwa Uholanzi. Mkewe hakuwa na lakufanya akamkaribisha mgeni na kumwandalia chumba cha kulala. Huyo dada ametokea Afrika ya Kusini anasema wakati wakisoma alipenda kutembelea Tanzania na aliomba huyo mume awe mwenyeji wake na alipofika walikwenda kutembelea mbuga za wanyama kwa muda wa siku 4 wakarudi na yule dada ameondoka amerudi kwao South Africa. Sasa yule mke anasema ana wasiwasi yule ni kimada wa mumewe amejaribu kumwuliza mumewe kuhusu huyo dada lakini mpaka sasa mumewe anasema ni rafiki amependa kutembea Tanzania
ananiomba nimpe ushauri maana yeye haamini jibu
nisaidieni wanaJF
Jana usiku amekuja rafiki yangu ameolewa na ana watoto 2 wiki mbili zilizopita mumewe alikuja na mgeni mwanamke nyumbani bila taarifa kwa mkewe akamtambulisha ni mwanafunzi walisoma nae wakati akiwa Uholanzi. Mkewe hakuwa na lakufanya akamkaribisha mgeni na kumwandalia chumba cha kulala. Huyo dada ametokea Afrika ya Kusini anasema wakati wakisoma alipenda kutembelea Tanzania na aliomba huyo mume awe mwenyeji wake na alipofika walikwenda kutembelea mbuga za wanyama kwa muda wa siku 4 wakarudi na yule dada ameondoka amerudi kwao South Africa. Sasa yule mke anasema ana wasiwasi yule ni kimada wa mumewe amejaribu kumwuliza mumewe kuhusu huyo dada lakini mpaka sasa mumewe anasema ni rafiki amependa kutembea Tanzania
ananiomba nimpe ushauri maana yeye haamini jibu
nisaidieni wanaJF
Kutokumfahamisha kwamba kuna mgeni haitoshi kumtilia wasiwasi!Kama kweli hakumfahamisha kwasababu anatoka nae hata kwake asingemleta!Angemlaza hotelini aage kiujanja waende zao safari!Inawezekana huyo mzee haoni kama mkewe ana sauti kwenye ndoa yao!Nyumba ni yake..maamuzi ni yake kwahiyo anaona anachoamua yeye ndicho..haoni haja ya kumshirikisha mkewe!Huyo mama badala ya kutuhumu asiyoyajua angemuuliza tu mumewe tena kwa utaratibu..Kwanini hakumjulisha kwamba kutakua na mgeni?Hilo tu!
Wkt mwngne wadada2nakarbsha stress wnyewe!