WanaJF ingilieni kati

WanaJF ingilieni kati

Joined
Aug 22, 2015
Posts
68
Reaction score
17
Habari zenu ndugu zangu? naombeni ushauri: Mimi nimeacha kazi baada ya kupata kazi ambayo imenigharimu muda na akiba yangu yote ya pesa ili kuipata, sio kwa kuhonga...bali kwa shughuli mbalimbali k.v. usafiri, printing, research n.k. Sasa hapa nilipo sina hela ya kuishi hadi mwisho wa mwezi mshahara utakapotoka na nina familia.

Tayari nimeshakopa kiasi kikubwa tu kwa mtu wangu wa karibu ambacho nilikitumia katika harakati za kutafuta kazi. Sasa nifanyeje? nimewaza kuhusu kumkopa bosi au mfanyakazi mwenzangu, naona nitaharibu credibility na kutengeneza maswali yasiyo ya lazima, hivyo lazima nilinde hii kazi kwa gharama hata ya kulala njaa...lakini kiuhalisia, siwezi kulala njaa hadi wiki 3 zijazo, hivyo nahitaji pesa.

Nimewaza kuhusu kuuza hii simu, napata wakatu mgumu kwasababu yenyewe ndio inanisaidia hata sasahivi kuwaambieni nyinyi ili mnipe mawazo.

Nimewaza kwamba labda mtu anawezajitolea kunikopa kwa riba flani kutokana na kiwango mshahara wangu, tukaandikishana kwa M/kiti, na mwenye nyumba wangu pamoja na familia yangu wawe mashahidi. Document nilizonazo ni k.v. mkataba wa kazi, kitambulisho, vyeti na cv yangu inayoonyesha utendaji kazi wangu mzuri na wa kuridhisha kiasi cha kuweza kuishawishi kampuni hiyo kutengeneza position ya kazi yangu maana hawakuwa nayo mwanzo...ingawa walikuwa wanahitaji huduma kama yangu.

NIFANYEJE???😥😥😥
 
Kama huna hii ya vocha je umetoa wap su ingekusaidia??
 
Yaani kwa akili yako yote ukaona hapa ni mahali sahihi..
 
kwa niaba yangu na wachangiaji wengine ndugu ungekuwa muwazi una uhitaji wa kiasi gani cha fedha. Pia security unazowekavyema ikilingana na kiwango cha pesa unchohitaji.
 
Hii Jf balaa, mkuu hapa asilimia 98 tunashindia mihogo sasa huo mkopo tutautoa wapi siye. Kaza buti kaka au ukajiunge na vicoba mtaani hapo.
 
Mkuu.......wife vipi......?.....nae kafulia........?........
 
Habari zenu ndugu zangu? naombeni ushauri: Mimi nimeacha kazi baada ya kupata kazi ambayo imenigharimu muda na akiba yangu yote ya pesa ili kuipata, sio kwa kuhonga...bali kwa shughuli mbalimbali k.v. usafiri, printing, research n.k. Sasa hapa nilipo sina hela ya kuishi hadi mwisho wa mwezi mshahara utakapotoka na nina familia.

Tayari nimeshakopa kiasi kikubwa tu kwa mtu wangu wa karibu ambacho nilikitumia katika harakati za kutafuta kazi. Sasa nifanyeje? nimewaza kuhusu kumkopa bosi au mfanyakazi mwenzangu, naona nitaharibu credibility na kutengeneza maswali yasiyo ya lazima, hivyo lazima nilinde hii kazi kwa gharama hata ya kulala njaa...lakini kiuhalisia, siwezi kulala njaa hadi wiki 3 zijazo, hivyo nahitaji pesa.

Nimewaza kuhusu kuuza hii simu, napata wakatu mgumu kwasababu yenyewe ndio inanisaidia hata sasahivi kuwaambieni nyinyi ili mnipe mawazo.

Nimewaza kwamba labda mtu anawezajitolea kunikopa kwa riba flani kutokana na kiwango mshahara wangu, tukaandikishana kwa M/kiti, na mwenye nyumba wangu pamoja na familia yangu wawe mashahidi. Document nilizonazo ni k.v. mkataba wa kazi, kitambulisho, vyeti na cv yangu inayoonyesha utendaji kazi wangu mzuri na wa kuridhisha kiasi cha kuweza kuishawishi kampuni hiyo kutengeneza position ya kazi yangu maana hawakuwa nayo mwanzo...ingawa walikuwa wanahitaji huduma kama yangu.

NIFANYEJE???😥😥😥

Njoo nikukopeshe kwa muda mkuu kama unatoa riba. Uwe tayari kutoa simu yako kama dhamana au kitu kingine cha thamani.
 
Pole!! Unahitaji Kiasi Gani?? Kma Unayo Mali Yyote Ya Thaman Na Pesa Unayohitaji, Fanya Uni Pm. Kingine Pia Unaweza Kukopa Kwa Mtu Wako Wa Karibu.
 
Sehemu nyingi za kazi mara tu unapoanza kazi kampuni hutoa pesa ya kujikimu.Hebu jaribu kufuatilia kama na wao hutoa,ukishindwa mweleza boss khs hali halisi atakuelewa tu.Haya mambo yapo sana ndio dunia ilivyo.
 
Mkuu.......wife vipi......?.....nae kafulia........?........

Mpka Amekuja Hapa, Unategmea Nn?? Japo Sio Nzur Sanaa Kw Swala Lake...Ingekua Poa Kwanza Kma Angewafata Watu Wake Wa Karibu Anaojuana Nao, Nampa Fursa Kma Anayo Mali Ya Kuweka Bondi Kwa Pesa Anayohitaji Sawa!!!
 
Ndio maana wenzenu hupenda kuoa ma baamed sbb ni wabunifu wa maisha.. huwazi mambo madogo madogo hata mshahara ungetoka tarehe 39.
 
Pole mkuu utasaidika tu,ukiona mambo yanazidi kua magumu ujue Neema iko karibu
 
pole sana ndugu.ELIMU UMEKOPA,KAZI UNANUNUA,yaani nchi yetu hadi raha sometimes,nakushauli usiendelee kukopa pesa kwa watu binafsi,maana itafika mwisho wa mwezi mshahara wote utaishia kwenye madeni ingawa sijui unapokea kias gan kama take home,jaribu ku uza samani za ndani kama unazo hata kwa bei ya hasara ikuwezeshe kwa muda,alaf ukijpanga utanunua tena,hiyo haina pressure yoyote,kama una tv,radio,viti,kitanda lakin sio godoro,jiko la ges au umeme,meza n.k.ama nenda bank ndogondogo kama advance bank,akiba,access n.k au taasis ndogondogo za mikopo km tujijenge,finca,platinam,bayport n.k,kakope hata laki 5 kwa miez 6,utarudisha riba ya laki 1 had lak na nusu kwa DHAMANA ya kazi tu,naamini kwa uzoefu wangu ndan ya siku 7 watakupa pesa.ukfanya moja kat ya hayo mawil,amin usiamin hautakua na pressure isiyo ya msing maana hakuna ataekupgia sim kukuliza pesa yake,wala hutakua na hofu na tarehe znavyosogea.try to think twice about these two things then let your nearest people to advise u abt ths bfore u carry forwad
 
MN Productions,

Umejaribu kutafiti hapo ofisini kwenu hamna kitu kinachoitwa salary advance? Salary advance ni jambo la kawaida sana kwenye ofisi nyingi zinazojitambua manake wanafahamu emergency kwa mfanyakazi ni jambo la kawaida na ili kumweka kwenye right track wakati wote, ndo maana huwa wanaweka hiyo huduma!
 
Last edited by a moderator:
MN Productions

Nakushauri kama unatumia line ya voda basi jiunge na m pawa then ingiza akiba ya elfu 10 kupitia m pesa, baada ya saa 24 watakuruhusu kukopa hadi laki 2. Na ikiwa utaweka akiba kubwa zaidi kwenye account yako ya m pawa ndivyo utakavyopata mkopo mkubwa zaidi

#VodacomKaziNiKwako
 
Last edited by a moderator:
itakupasa uweke kitu chako bondi/poni dukani kwa mangi akupe sente za kusogeza siku...
 
Back
Top Bottom