Kamanda wa Kweli
JF-Expert Member
- Jul 13, 2014
- 1,448
- 845

Rais Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud amesema kuwa takriban wanajeshi 180 wa Kenya waliuawa katika uvamizi wa kambi yao huko El Ade na wapiganaji wa kundi la Alshabaab.
''Wanajeshi wa kigeni hufariki na hatuendi katika mazishi yao.Wakati wanajeshi 180 ama 200 wa Kenya waliotumwa nchini Somalia na sababu ya kutumwa kwao nchini humo ni kuleta udhabiti kuwaisaidia raia wa Somalia na wanauawa alfajiri moja, si swala la kawaida kwamba wageni wameuawa.
Kile kilichosalia ni kwamba jamaa zao walielezwa kwamba kulikuwa na vita na watu wao wakafariki kutokana na hilo'',rais huyo alinukuliwa akisema hivyo katika kituo kimoja cha runinga nchini Somalia.
Chanzo: BBC Swahili