Wanahabari wasitumie taaluma yao kuwachonganisha raia wema na serikali yao.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kumezuka mtindo mbaya sana wa waandishi wa habari wa magazeti, watangazaji wa redio na luninga kutoa habari kupitia vyombo vyao wakiwaandika na kuwatangaza wahanga wa matukio mbali mbali kuwa wanaitambia serikali.

Kwa mfano, wataandika "mtuhumiwa huyo wa makontena amesema anajuana na wakubwa kwa hiyo hakuna wa kumfanya kitu" au "msimamizi wa ujenzi huo amesema hatavunja gorofa hilo kwa sababu ameishaiweka serikali mfukoni"

Lakini kiuhalisia utakuta hakuna mhanga yeyote mstaarabu anayeweza kutamka maneno ya kipumbavu kama hayo isipokuwa kauli kama hizo huwekwa ama kuchomekwa kwa makusudi na mwandishi au mtangazaji ili tu kumchafua, kumgombanisha na kumjengea picha mbaya mhusika kwa serikali na jamii.

Ni vema kama waandishi na watangazaji wa habari kama hizo watatoa sauti za mahojiano na watu hao wakiyatamka maneno hayo badala ya kuandika majirani waliohojiwa wametuambia kwamba mmiliki kasema hivi na hivi huku wakijua hakuna mtu aliyewaambia maneno hayo.

Nadhani ni jambo jema kama wanahabari watakuwa waadilifu, wakweli na wawatendeao haki watuhumiwa wa jambo lolote badala ya kuwachomekea kauli zinazojenga chuki.
 
Last edited:

Huo ndio tunauita ukanjanja, na wanaowapa kiburi ni wahariri kwani na wao elimu zao ni mashakamashaka. Sekta ya habari inahitaji mabadiliko makubwa sana, kibaya zaidi wanahabari wa nchi hii wanajiona wanahaki ya kukosoa sekta nyingine ila wao wakiguswa wanaanza kulalama hovyo.
 
Back
Top Bottom