kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Watoto hawana wanachokifahamu zaidi ya kupokea kile wanachopewa. Elimu ni kama ibada haitaki najisi. Watoto ndio taifa la kesho, hivyo kuwapatia elimu wote ni gharama kubwa isioepukika wala kuwa na mbadala. Watoto wetu sasa hawana muda wala utulivu wa kuzingatia masomo kwasababu zinazoepukika kabisa.
Wako waliokosa mikopo, wako waliopewa mikopo lakini pungufu, wapo wanaotakiwa kuhakiki taarifa zao upya, wako waliokosa sehemu za kukaa hostel, wako walitolewa madarasani kwa kukosa ada, wako walikatazwa kufanya mitihani, wako walionyimwa matokeo ya mitihani kutokana na kudaiwa ada, wako waliorudishwa nyumbani, wako wanohama vyuo kufuata ada nafuu vyuo vingine, n.k. Mambo yote haya yanawatoa watoto wetu kwenye reli ya kusoma, kujisomea na kujifunza. Kila mtoto ameingiwa na hofu ambayo sisi wazazi wao hatukuwa nayo tulivyokuwa wanafunzi. Sisi wazazi tulisoma vizuri sana tena wengine buree kabisa na hata siagi za mikate tulipewa bure.
Kadhia kama hizi kwa watoto wetu zinaweza kuwapunguzia ari ya kupenda masomo na kupoteza uzalendo wao kwa taifa lao ambalo ndio wanalotarajia kuja kulijenga huko mbeleni baada ya kuhitimu masomo yao.
Nashauri chondechote, tuwape watoto wetu wenye sifa elimu bila ya mashariti, usumbufu, na masimango ili watulize akili zao kwenye masomo wakati tunapohangaika na ufisadi wa viongozi waliopewa dhamana na mifumo mibovu inayotoa mianya ya upotevu wa mapato yetu.
Ni heri tuziuze pembe zetu zote za ndovu wetu ili tugharimie elimu za watoto wetu badala ya kuzichoma moto huku watoto wakikosa elimu kwa kigezo cha bajeti finyu. Wazungu huwa wanatucheka sana kumuuona mtu masikini akichoma moto mtaji na kukimbilia kwenda kukopa fedha kwao! (eti masikini jeuri).
Taifa liketi kuamua hatima yake.