Ninasikitishwa sana na hili tatizo, kwa wanaofuatilia hakika watakuwa wameshaligundua hili tatizo.
Katika uchunguzi nilioufanya niligundua kuwa wanafunzi waliofanya vizuri sana tena kwa jitihada BINAFSI zao na walimu katika shule za msingi za serikali hawakuchaguliwa wote kwenda shule za bweni ukilinganisha na shule za msingi za "PRIVATE" kwani wao wamechanguliwa kwa wingi sana kwenda shule za bweni.
Ukiuliza kwanini inakuwa hivyo majibu mepesi utakayopata ni kwamba nafasi za bweni ni chache, pili wanafunzi wa shule BINAFSI wamefaulu vizuri zaidi.
Hizo sababu haziendani na hali halisi ukilinganisha shule za umma na BINAFSI, angalia mazingira kwa ujumla ambayo watoto hawa wanasomea ktk shule za umma na BINAFSI kisha linganisha,mazingira hayaendani kabisaa!
Pili,uwezo wa kifedha wa wazazi wa watoto(wfz) hawa katika pande zote mbili, utagundua kuwa wanaosomesha watoto wao shule za private wanouwezo wa kuwasomesha watoto wao piahata shule za private za bweni.
Tatu,linganisha idadi ya wanafunzi wanaosoma katika darasa moja katika shule za umma na BINAFSI,utakuta shule za umma darasa moja lina wanafunzi kwa wasitani wfz 80 ambapo private kwa wastani darasa moja lina wfz 40. Ufundishaji na ujifunzaji unakuwa mgumu sana shule za umma.
Nne,vifaa vya kufundishia na kujifunzia,vifaa ktk shule za umma ni chache/hafifu na duni huku private ni vya kutosha na ni bora.
Tano,Walimu; shule za Umma walimu ni wachache, hawaendani na idadi ya wanafunzi ingawa ni mahiri sana kuzidi wa private,ambapo shule BINAFSI walimu ni wengi na wanafundisha wanafunzi wachache.
Sita,Mishahara kwa walimu na mazingira halisi ya kufanyia Kazi, walimu shule za Umma wanafanya Kazi ktk mazingira magumu sana ikiwemo mishahara midogo isiyokizi mahitaji yao ya kila siku,ukilinganisha na walimu wa shule za private na bado wanajituma kufundisha wfz hadi kufikia kiwango cha shule za private ambapo wao changamoto ni kidogo mno!
Kwahiyo kutokana na baadhi ya sababu hizo,inakuwaje unawashindanisha HAWA wfz ili hali huduma wanazopata hazilingani !!!!
Sababu kuu nyingine ambayo baadhi ya shule za private zinatumia ni KUIBA MITIHANI NA KUWAFANYIA WANAFUNZI ili wafaulu vizuri wavutie wateja na biashara iwe nzuri, Hii ni biashara bhana!
Hebu fikiria tu kidogo katika hali tu ya kawaida ya uelewa wa kila binadamu inawezekanaje shule x ya private inawanafunzi 60,wote wakafaulu kwa ufaulu unaofanana? Kila somo A na Wastani wote wakapata A.
Sasa kuna matokeo nimeyaona kuna wanafunzi wa shule za umma, wamefaulu vizuri sana, wana A 4/5 na wastani wa ufaulu ni A ya 45/50 kila somo, lakini hawajachaguliwa kwenda shule za bweni.
Serikali awamu ya tano,serikali makini na yenye kuaminiwa na wananchi wote,Nawaomba mliangalie hili hakikisheni kwanza watoto wa maskini waliofaulu vizuri na kupata sifa ya kuchaguliwa kwenda sekondari za bweni wanachaguliwa wote na kisha wa shule za private!