Gypsum Screw
JF-Expert Member
- Jun 10, 2024
- 1,393
- 1,577
Tangu uhuru taifa limekuwa likiongozwa na wao. Kila siku hatuachi kukumbushwa juu ya mazuri na mema mengi sana ambayo wametufanyia (utadhani ni hisani). Hapa utasikia mambo kama tumejenga shule, tumejenga barabara, tumejenga hospitali, tumeleta umeme, tumeleta hiki na kile.
Sasa basi, katika muktadha huo wasiwasi wa mabadiliko ya kuruhusu watu wachague viongozi wanaowataka katika mazingira ya haki na usawa unatokea wapi?
Unasema umewapa watu maendeleo, huku makundi mbalimbali yakijitokeza kuchagiza na kumwagia sifa hata asizostahili yule mgombea aliyejipisha mwenyewe huko chama kinachotawala ili kuonesha kwamba wanampenda sana.
Sasa kama wameleta maendeleo mengi kiasi hiki na watu wanampenda sana mgombea aliyejipitisha mwenyewe huko chama kinachotawala, uoga wa kuacha watu wawachague kwa uhuru na haki ni wa nini?