Wana jamvi heshima kwenu naomba kujua process za kutoka nchi hii maana naona ni miyayusho tu natamani nizamie Korea kusini huko

zyuho

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
242
Reaction score
385
Kama kichwa hapo juu kinavojieleza Mimi ni muajiriwa wa shirika kubwa tu la serikali hapa nchini (temporary Employment) miaka 9 sasa naona wazo linalo nijia mafanikio yangu hayatapatikana kwenye nchi yangu ya ahadi sasa natamani nikapate changamoto mpya kwenye nchi za watu.Naomba ushauri wenu wakuu wa process za kuvuka ng'ambo ugumu na njia zake ni zipi. PM iko wazi kwa ushauri wakuu
 
Changamoto zipo kila mahali. Hata walioko Korea Kusini wanatamani kurudi Tanzania.
 
Ingia tovuti ya uhamiaji jaza details zinazotakiwa kupata hati ya kusafiri nje ya nchi hakikisha uwe na NIDA na cheti Cha kuzaliwa nafkir utalipa 30,000/= zikikamilika utaziprint.

Baada ya hapo utahitajika kwenda kupiga picha kwenye ofisi ya uhamiaji na kuziacha zile karatasi ulizoprint hapo nafkir utalipa 120,000/= na ndani ya wiki mbili passport Yako itakuwa tayari.

Kama huna idea ya wap Kuna maisha wakati upo uhamiaji angalia watu piga nao stori unaweza pata pakuanzia.

Fikiria kisiwa Cha Mayotte kipo hapo jirani mbele ya Comoro kipo chini ya imaya ya mfaransa ni rahisi Kuanzia hapo ikiwa n junction ya kwenda nchi za umoja wa ulaya endapo utafanikiwa kupata Visa pia uzuri wa Mayotte maisha ni ya kiafrika na waswahili utawakuta ila usisahau malengo yako
 
Tafsiri yako ya mafanikio ni ipi ?
 
Hakikisha kwanza unaweza kuishi bila dini wala imani yoyote maana huko hayo mavitu yamepigwa marufuku na uwe teyari kunyongwa ukishindwa kulipa kodi
 
Njia nyepesi isiyo na mambo mengi ila uwe mvumilivu zamia kwenye kambi yeyote ya wakimbizi, huko utasubiri kwa muda upate nafasi ya kwenda mbele japo yaweza isiwe huko Korea kusini
 
Hivi unapotaka kuzamia nchi fulani kuna process inafuatwa kutoka kwenye nchi unayotoka?
 
Nje nje nje ndani! popote kambi baba weka Maskani....'Gangwe Mob"...Inspector Haroun vs Luten.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…