Wana-CHADEMA na watanzania wangapi mnajua hili?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kwamba, Dr.Kitila Mkumbo aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA hadi 2010. Alijiuzulu nafasi hiyo mwaka 2010 na tangu hapo hakuwahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Kwamba, tangu 2010 Dr.Kitila Mkumbo alikuwa akitumiwa na CHADEMA kama Mshauri tu na si Mjumbe wa CC ya chama hicho.

Kwamba, si kweli kabisa kuwa Dr.Kitila alivuliwa Madaraka yake ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kwakuwa kwa mwaka 2013 hakuwa tena Mjumbe wa CC kwakuwa alikoma kuwa hivyo tangu 2010. Asingeweza kuvuliwa cheo asichonacho.

Kwamba, suala la kujiuzulu kwa Dr.Kitila Mkumbo,tangu 2010,limekuwa halijulikani na hivyo kupotoshwa kwa kumwita Mjumbe wa CC hadi 2013.

Mambo haya yamebainishwa na Dr.Kitila Mkumbo pamoja na shahidi wake ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA,Ndugu Antony Komu. Yalisemwa hayo tarehe 21/3/2014 wakati wa Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya UDSM.

Chanzo: Mmoja wa Wajumbe wa Kikao hicho cha ndani ya UDSM.
 
Mbona unarudisha haya ma issue au matokeo ya Kalenga kwa chief Mkwawa?
 
Komu tena? Kama ni kweli, taratibu za chama zichukue mkondo wake kwa kukata pande zote.
 
Hilo linaingia akilini kwani huyo Jamaa ni mwajiriwa wa Serikali na sheria ya zinamkataza kuwa mwanachama wa Chama cha Siasa. Japo ukweli ni kuwa wale wanaokatazwa na sheria kuwa wanachama wa vyama vya siasa wao ni wanasiasa kweli kweli.
 



Watajulia wapi wakati wapo kwenye viroba saaa zote ..
 
So what!! Kushindwa kuwandle wasomi ni dalili mbaya kwa CDM.moja ya changamoto kubwa tuliyonayo Africa ni kutokuthamin nafas ya utaalamu kwenye maamz matokeo Yake wamewekwa pembeni. Nikidhani CDM imeliona hili na kuamua kuwatumia wasomi Kama akina kitila lkn kumbe na chenyewe kiko na mlengo ule ule wa kuwaona wasomi kma watu wasio na umhimu wowote.

Kwa ss ambao Tuko nje ya CDM, ni vigumu kuelewa Kuwa ule waraka uliokuwa na model iitwayo SWOT analysis ndio iliyomfukuzisha, wakati Hiyo ni mgt tool ya kusaiidia mgt iondoe weaknesses kwa kutumia strength na threats kwa kutumia opportunities.

Hiyo ingewasaidia kma taasis kujipima na hatimaye kusonga mbele.
 
Hilo linaingia akilini kwani huyo Jamaa ni mwajiriwa wa Serikali na sheria ya zinamkataza kuwa mwanachama wa Chama cha Siasa. Japo ukweli ni kuwa wale wanaokatazwa na sheria kuwa wanachama wa vyama vya siasa wao ni wanasiasa kweli kweli.

nijuacho mimi ndugu sheria haikatazi kuwa mwanachama wa chama cha siasa ila inazuia kushika wadhifa wowote wa chama cha siasa ukiwa mwajiriwa wa umma na pia kuendesha shughuli zozote za kisiasa ukiwa eneo la kazi,naomba tafsir ya hii sheria kwa anaeijua vizur kwa sababu naona inatumika kwa vyama vingne tu ila sio kwa ccm,vp hii imekaaje
 

Nitafurahi kupata tafsiri sahihi ya uelewa huo kwa kuwa mimi mwenyewe sina kadi ya chama chochote cha siasa kwa kuwa mwajiri wangu alituambia haturuhusiwi kujiunga na chama chochote cha siasa. Hii ndo maana akina sisi tunapenda hoja ya mgombea binafsi ipite ili sisi tuliofungiwa haki zetu za kikatiba cha kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi za kisiasa tuzipate.
 
Tatizo ni kuwa hata Kitila mweyewe alikuwa hajui hadi alipopata mgogoro chuoni alikokuwa anafundisha. maana ndipo tulipoanza kuzisikia hizi simulizi.
 
Inamaana kile kizee kilikuwa hakina taarifa wakati anatangaza kuwafukuza?
 
Wanavuta shuka asubuhi kalenga tayari subirini chalinze
 
Inamaana alijiuzulu bila kujua?
Si alisema baada ya kuhojiwa na CC alikuwa waliomba kujiuzulu yeye na Zitto ila Tundu Lissu kapinga? Hili si alisema mwenyewe au alikuwa anaomba kujiuzulu cheo hichohicho kwa mara ya pili?
Kama kweli ndio kasema haya tena basi tunahaja ya kutilia shaka kuu kumbukumbu zake!
 
Anajitetea kisheria zaidi,huwezi kukubali kuwa wewe ni mwizi hata kama kweli umeiba.:
 
Kwahiyo unataka tufanyeje ?hayo mambo tulishayamaliza tunasonga mbele tumeweza kwa mara nyingine kuvuka kizuizi cha nyinyiemu tunajiandaa kwa vingine zaidi tuko gado tuko kamili na Mungu yu pamoja nasi
 

hata mim nilidhan wangetumia waraka huo kama sehemu ya kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…