Wamoja katika pesa, watengefu katika imani, imekaaje hii?

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,219
1,280
Wana JF,

Hebu tutafakari kidogo katika hili, inakuwaje kuna dini nyingi lakini zinahubiri Mungu mmoja? Tena zingine zinatufanya tusishirikiane kwa baadhi ya desturi za maisha mfano, katika vyakula, mavazi, namna ya kuabudu, mazishi nk, lakini ajabu niionayo mimi ni pale wote hawa wanapotumia pesa moja bila kubaguana! Mfano, kwanini hakuna utaratibu wa kusema hii 500/- uliyonipa ni ya kikrito ili hali mimi ni muislam/mpagani ama kinyume chake! Kwanini ufuasi wa Mungu unawafanya watu watofautiane katika imani na wakati huo wote wanafanywa kuwa wamoja katika pesa? Wenzagu mliwahi kuwaza haya? Karibuni kwa fikra njema za kutufanya kuwa wamoja.

Sorry kwa watakaokwazika kiimani!
 
Great thinkers vp? Kwikwikwikwikwiiii!!!
 
Kuna watu waliniaminisha jf ni kila kitu, u can ask anything, hapa mnaniangusha!
 
Kwani halijibiki kiimani, kitaalam au kiuchumi?
 
Baada ya kuhangaika huku na kule na kukosa majawabu ya swali langu, bila shaka binafsi naweza kufafanua nilichokifikiria tangu nimeuliza mpaka leo maana hata Great thinkers walikimbia!
Kwamba, jambo lolote ambalo mwanadamu anaweza kulifanyia utafiti hasa wa kisayansi na kuonyesha kuwa ndivyo lilivyo na si vinginevyo, basi jambo hilo watu wote watakuwa wamoja tu! Masuala yote ambayo yapo na hayawafanyi watu kutengana kiimani hayawezi kuepukika kwa mustakari wa maisha yao na mfano mzuri ni matumizi ya pesa! Hii ni Dunia nzima watu ni wamoja katika pesa, hakuna pesa maalumu kwa Mkristo, Muislam wala mpagani!
Hakuna Sayansi ama Technolojia inayoweza kutoa jibu la imani gani sahihi kwa watu wote na ndio maana kila kunapokucha dini na madhehebu kwa kila imani vinaongezeka!
Ahsanteni na karibuni kwa michango yenu zaidi!
 
Nimeufukua tena uzi huu nikiamini kuwa, kuna great thinkers wengine wengi hawakuuona kipindi naweka uzi huu, karibuni kwa mawazo mbadala!
 
Back
Top Bottom