Wameru walivyomkataa Mkapa mwaka 1995

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
nimeshtushwa kusikia kwamba aliyefungua kampeni huko arumeru mashariki ni mheshimiwa rais mstaafu ndugu benjamini mkapa.

Nimejisemea moyoni kwamba hiki chama nguli na kikongwe kimesahau historia?au ndio mambo ya vijana?

Kama kumbukumbu zangu hazijaathiriwa na uzee basi mtakubaliana nami kuwa mwaka tisini na tano kura za wameru zilienda kwa NCCR mageuzi ya mrema.mkapa alitoswa waziwazi na wameru.

Sasa leo hii miaka zaidi ya kumi na saba baadae tunadhani wameru wamebadulisha msimamo wao dhidi ya mkapa?

Leo hii ccm isilalamike jimbo likiangukia chadema kwani kuna makosa kadhaa yamefanyika ambayo yanaweza kuwaathiri katika uchaguzi huu.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom