Wamehukumiwa kwa ushahidi kidogo, ushahidi mkubwa ni kwa Mwenyekiti

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
haya ni mahojiano yaliyofanyika kwa wazee mbalimbali ambao walihusika na nafasi mbalimbali kwenye baraza na serikali ya kijiji iliyopita katika kijiji cha Tujivunie. Mwandishi alikuwa akiwahoji kutokana na wengine kuwa na kesi na wengine ni kwa vile ni wastaafu tu wa serikali ya kijiji iliyopita.

Mzee na 1. naitwa cha kushikiwa. Ndiyo, hili ni jambo linaloniumiza sana. walikuwa wawili mtoto na baba yake wakasema wamekuja kunisalimia. kwa kuwa utamaduni wetu kutembeleana na kusalimiana ni jambo la kawaida sikuwa na tatizo. Ukichukulia yule mzee aliuwa ndiye mzee wa kijiji alikuwa na ruhusa ya kutembelea watu wakati wote.
nliwakaribisha na tukawa tunaongea mara wakaona ng'ombe wa kijiji akiwa anapita wakauliza yule ng'ombe wa nani nikajibu ni wale ambao kijiji kimenipatia kuwatunza toka kwa wananchi wote kama mchango kwa kijiji kwa ajili ya kusaidiana. kiukweli alikuwa ng'ombe amenona wakasem basi wao watamchinja. wakamswaga mpaka bandani wakamchinja wakabeba nyama wakiniachia kwato,mapembe na ngozi ili nikaushe niifanye ya kukalia.
baada ya muda tena wakamtuma kijana mmoja wakisema ni ndugu yao nimpatie mbuzi. sikuweza kuzuia kwa kuwa hawa ni watu wakubwa kijijini kwetu. Sasa mwenyekiti wa kijiji amechaguliwa mwingine nimekuja kukamatwa kwa kuwa nimekutwa na ngozi ya ng'ombe wa kijiji. kiukweli mimi sikuua ng'ombe wa kijiji.

Mzee wa 2. Mimi naitwa mzee mashaka matupu. Nlikuwa nahusika na bwawa la samaki la hapa kijijini. mwaka jana mwenyekiti wa kijiji alisema kuwa yeye apelekewe kila siku samaki 5 kwa ajili ya mlo wa familia yake sikuweza kumkatalia maana yeye ndo aliniteua kwa nafasi hii. leo nakunja kukamatwa kwa kuwa nliruhusu jambo hilo litokee na kukutwa na magamba ya samaki nyumbani kwangu.kiukweli mimi nlikula dagaa wawili watatu tu lakini samaki wakubwa alichukua yeye.

Mzee wa 3. Mimi naitwa mikolo mingi. mimi nliteuliwa kushika nafasi ya uangalizi wa ardhi hapa kijijini kwetu. mwenyekiti yule alipenda kukutembelea nyumban kwetu kila mara na alianza kuwa akija anakuja na viroba ili achote mchanga kwenye kile kiwanja cha ujenzi wa hospital ya kijiji. sikuweza kumkatalia maana alinambia ue mchanga anautumia kujengea ofisi ya mwenyekiti wa kijiji kwa kuwa ile aliyokuwepo ilikuwa imechakaa. leo nakuja kukamatwa kwa kuwa kwenye kiwanja cha kujenga hospital ya kijiji kumebaki mashimo tu. nimeachiwa ushahidi wa mashimo.mimi sikuchota mchanga mwingi zaidi ya debe moja tu kuzibia nyufa kwenye nyumba yangu.

Mzee wa 4. mimi naitwa mzee twendeko migelo ni mwangalizi wa misitu na mali asili za kijiji. nimeumia sana maneno ya kuwa mimi nahusika na kusafirisha tausi,khanga na mbuni nimeyasikia. kiukweli mwenyekiti aliyepita siku moja alikuja kuangalia hawa ndege akasema kuna mwenyekiti wa kijiji cha mbali cha omarato alikuwa anahitaji dume la mbuni. hivyo anaazima akampandishe. walikuja vijana wakakamata wale mbuni,khanga na tausi wakaondoka nao. mimi sikuweza kuzuia. leo nimekuja kukamatwa kwa ushahidi wa manyoya tu ambayo nliachiwa ili kupamba nyumbani kwangu.

Mzee wa 5. mimi ni mzee akili nyingi sina la kusema yote namwachia mungu

Mzee wa 6. jina langu la nini? hamna kazi ya kufanya? niacheni mimi nishughulike .

Mzee wa baraza la kijiji. naitwa bakari maembe. huyu mwenyekiti wa kijiji mpya sioni
anachofanya. kiukweli namwona yupo yupo tu. ametusahau sisi wakongwe wenye uzoefu kwnye kulitumikisha taifa hili. anadhan akishinda ndani tu inamsaidia. aende kuzunguka zunguka atuulize sisi wenzie tulitembelea vijiji vingi hapa nchini. huko kote tunafahamika na tulimwaga mbegu. nawaambia atashindwa tu.
wazee mbali mbali wataendelea kutoa ushuhuda kuhusiana na mambo mbali mbali waliyotenda na wanayotendewa sasa na mwishowe kutoa ushuhuda.
 
Hivi kwanini Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mbya hazijaguswa? Kila kitu Dar huko hawapaoni?
 
Back
Top Bottom