Walisajiliwa Yanga, Wapitishwa na CAF kucheza kombe la shirikisho

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limepitisha majina ya wachezaji wanne wapya wa Yanga, kipa Benno David Kakolanya, Hassan Hamisi Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew Chikupe na Juma Hassan Mahadhi kucheza Kombe la Shirikisho.Yanga inafungua dimba na Mouloudia Olympique Bejaia Juni 19, mwaka huu, Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria na sasa wanne hao wako huru kucheza.

Yanga ambayo imeweka kambi katika hoteli ya Rui mjini Antalya, Uturuki tangu Jumapili na itaondoka kesho kwenda Bejaia kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wametumiwa leseni za wachezaji hao kutoka CAF.

Hassan Kessy (kushoto), Juma Mahadhi (katikati) wakiwa na Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh wakati wa safari ya Uturuki “CAF imetuma leseni za wachezaji hao wanne wapya wa Yanga na maana yake sasa wako huru kucheza Kombe la Shirikisho,”amesema Mapunda. Kakolanya amesajiliwa kutoka Prisons ya Mbeya, wakati Kessy ametoka kwa mahasimu, Simba, Vincent ametoka Mtibwa Sugar na Mahadhi ametoka Coastal Union.

Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco, Bouchaib El Ahrach atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk. Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kuwakaribisha mabingwa wa Afrika, TP Mazembe Juni 28 katika mchezo wake wa pili wa Kundi A. Na katika mchezo huo, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limechanganya marefa kutoka nchi tatu tofauti, ambao ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na Berhe O'michael wa Eritrea.

Timu nyingine katika Kundi A ni Medeama ya Ghana ambayo itafungua dimba na TP Mazembe mjini Lubumbashi Juni 17, mwaka huu, mchezo ambao utachezeshwa na marefa wa Shelisheli Bernard Camille, Hensley Danny Petrousse na Eldrick Adelaide.

Kikosi kamili cha Yanga kilichopo kambini Uturuki ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya. Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' na Bossou anayetarajiwa kufika leo.

Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya. Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe. Msafara upo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.
 
Mzigo unapigwa kesho, mnaoipenda hiyo timu muende kuipokea ikirudi kuonyesha mshikamano bila kujali matokeo ya kipigo ambayo ni haki yake.

Sisi tutachekea chooni
Nakuonea huruma! Utakufa kwa kijiba cha roho!
 
haaa haaa muosha huoshwa ....vialaza ndio lugha gani tena? eti vialaza, hell no...@sanif
Ukitaka niandike unavyotaka wewe ungeona nyota nyota badala ya hilo neno ndio maana tunapindisha kidogo,wenye kujiongeza washanielewa kazi kwako k..ilaza
 
Ukitaka niandike unavyotaka wewe ungeona nyota nyota badala ya hilo neno ndio maana tunapindisha kidogo,wenye kujiongeza washanielewa kazi kwako k..ilaza

hakuna aliyesema uandike kama nitakavyo mimi, mbona na we umekuja hapa na matakwa yako kwa kukosoa aliyeandika CUF, acha ujuaji na kubali kuwa kuna typing errors hasa kama unatumia "simujanja" za siku hizi... mbona na wewe hukujiongeza kwa makosa ya mtoa thread...Over and out.
 
Angalia ilipo A na U halafu uone typing error inawezekena vp kwa hicho alichoandika
 
Mkiambiwa vialaza mnakuja juu,eti CUF

ukiangalia herufi zilipo katika keyboard utakuwa unakosea, chukulia ulichoandika wewe "vialaza" A imejipachikaje hapo wakati I na L zipo mbali kabisa....admit kuwa typing errors are there ....mkuu usipaniki lengo ni kusaidiana tu.
Viva Young Africans Sports Club/Yanga Afrika.
 
Inaonekana hujaelewa,ni hivi hilo sijakosea nimeandika makusudi maana ningeliandika kama lilivyo siku za hivi karibuni mods wanalifuta ndio maana nimeliandika hivyo au mgeni humu ndugu,ebu jaribu kuliandika uone
 
Singular: KILAZA .....Plural: VILAZA... haya let see what will happen
 
Back
Top Bottom