Waliosoma diploma ya computer science IFM.

Rchesse

Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
60
Reaction score
28
Kwa wale ambao wamesoma diploma ya CS IFM naomba mnipe ushauri.

Nimemaliza form four 2018. Div 2-18. Nime apply cert ya information and technology kwa lengo la kuja kusoma diploma ya CS hadi degree. Nilikuwa sijafanya utafiti sana nikawa nafikiri CS mnakuwa mnafanya mambo ya software development tu. Lakini baada ya kufanya utafiti nikagundua kuwa CS ina math ngumu, namimi nilipata D kwenye math kwasababu nilikuwa sio muudhuriaji mzuri. Sasa nahisi hii itakuwa kikwazo kwangu. Sasa nilikuwa nauliza IFM wana focus sana kwenye math? (kwasababu nasikia inategemeana na chuo), pia nilikuwa nauliza mnanishauri nisomee IT au ICT au nikomae na CS.
 
Cs ndo IT yenyewe sasa, komaa utoboe
 
Mathe inategemeana na chuo? Math ni msingi wa CS ni kama engineering lazima math, ukitaka uwe mbobezi katika CS ni lazima uwe vizuri sana tena sana kwenye math.
Computer scientists hawa ni watatuaji wa matatizo kwa kutumia algorithms na mathematics kwa msaada wa komputa, tell me unakosaje kusoma hesabu ambayo ndiyo msingi wa CS.

Ushauri wangu kama unahuhakika upendi na uiwezi math narudia tena kama unahuhakika uiwezi na uipendi hesabu lakini unapenda kusoma kompyuta basi soma IT ambayo ndiyo hiyohiyo ICT.
Huko kwenye IT kupo generalised sasa wewe utaamua uwe expert kwenye nini manake kwenye IT kuna networks, security,programming(humu kuna hesabu ya kutosha), computer hardware and software maintainance and repairing, database administration, graphic design,nk
Pia fanya utafiti zaidi kwa haya tatayo kushauri ili uweze kupata uamuzi sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…