Waliofanikiwa kuishi mke na mume kwa dini tofauti walitoboaje?

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
1,077
1,426
Habari za jioni ndugu zangu wa JF.

Suala la mahusiano linavuruga akili kiasi cha kutesa sana.Macho yanaona msichana mrembo sana maishani kila siku.

Mrembo ulie muona aweza kuwa wa dini yako ama wa dini nyingine.Moyo ukadunda sana tena yawezekana kwa mlimbwende wa imani nyingine.

"Aaah potelea mbali".Moyo ukasema nampenda hivyo hivyo na dini yake tofauti.Huambiwi lolote ukasikia kuhusu dini.

Mara paap! Mpaka watoto wakazaa bado wameng'ang'aniana tu dini tofauti.

Waliopitia hili walitoboaje na uchambuzi pia unaruhusiwa.Aisee! Mapenzi haya.

Karibuni.
 
Ni udhaifu wako na kutojua maana ya dini. Waziri mkuu wetu ni muislamu na mke wake mkristo na wanadunda wakiwa ktk mafanikio ya juu. Mnaendekeza vitu vya kijinga wakati Mungu ni moja
 
Hakuna lolote la ajabu, uncle wangu alipata mke mwislam ikalazimika awe Islam maana alimpenda sana, akasema sawa na ndio ilikuwa siku ya kwanza na ya mwisho kuingia msikitini, mwaka wa 12 wanaishi vizuri kuliko mtu yeyote na kiti moto anapiga
 
Mimi nashauri hapa na iwe kwa manufaa ya wote watakaosoma hii,kwamba kama unaipenda sana imani yako na unajua ndiyo halisi itakayaoamua kesho yako na una option ya kumpata mwenza sawa na imani yako fanya hivyo.

Usiige walichofanya waliokutangulia linapokuja suala la kutafuta mwenza,utaiga kujenga utaiga kununua gari utaiga kulewa lakini life style ya ndoa haijawahi kuwa na copy ukifanya hivyo utateseka ufe siku si zako.
 
Familia kama hazina choko choko mnaishi kiroho safi ! Pia mambo ya kufunga ndoa kwenu isiwe priority mtaishi vizuri sana !! Kingine mmoja awe tayari kukubali kwamba watoto watafuata dini tofauti na yake !

Mama yangu mdogo aliolewa na mkristu huku yeye akiwa muislam ! Wako poa sana na mumewe ratiba zake za kusali zinaendelea kama kawaida watoto walifuata dini ya baba ambaye ni catholic wamekua kwenye maadili ya kikristu ! Walibalance vizuri sana !! Binti yao wa kwanza ana miaka 27

Wasumbufu ni wale misimamo mikali ! Ila wengi wetu dini ni majina tu ila hatuyazingatii sana
 
Ni udhaifu wako na kutojua maana ya dini. Waziri mkuu wetu ni muislamu na mke wake mkristo na wanadunda wakiwa ktk mafanikio ya juu. Mnaendekeza vitu vya kijinga wakati Mungu ni moja
Maisha kila mtu ana uelewa wake,ndiyo maana hata darasani wanafunzi hutofautiana ufaulu.
 
Back
Top Bottom