Waliodakwa na Magufuli kwa kuficha magari bandarini wafikishwa mahakamani

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,984
19,285
Ni watuhumiwa walioficha magari wakidai ni mitumba wamefikishwa mahakama ya Kisutu, habari hii nimeileta kwa kuwa kulikuwa na kuaminishwa kuwa hakuna waliokamatwa kwa kuficha Magari bali ni kiki ya kufunika habari za Nape

Tunashukuru kwa habari.

Ungeongeza kwa kutuambia walishikwa lini na walipelekwa mahakamani lini kwa mara ya kwanza.?
 
Hawa walishikwa na TPA toka siku nyingi..

Siku ile JPM ameenda port hawa jamaa tayari walikuwa tayari wana zaidi ya wiki pale kwenye selo za polisi bandari...

Acha kupotosha kwamba walidakwa na JPM...

JPM yeye alikuwa anapewa taarifa ya hili tukio lakini watuhumiwa walikuwa ndani tayari.
 
Mleta mada tunashukuru kwa updates. Ila pia nikusahihishe kidogo, hawa watu hawakushikwa na Mh. Rais ile siku alipotembelea bandari. Mh. Rais alikwenda kuangalia makontena yenye mchanga wa dhahabu ikiwa ni baada ya yeye kutoa zuio la ufarishaji wa mchanga nje ya nchi. Sasa katika yale ya ziada (AOB) ndipo akajulishwa moja ya mafanikio ya utumiajia wa scanning machine katika kuhakiki mizigo ni pamoja na ukamatwaji wa makontena yaliyokuwa yamebeba magari lakini documents zake zinaonyesha ni nguo za mitumba.
 
Acha upotoshaji wa kutafuta Kiki kwa JPM! Hakukamata yeye bali alionyesha na watendaji wa bandarini kwa maana ya TRA, BANDARI, NA TIKSI. Tena hakuwa na taarifa za hiyo issue yeye alienda kwa ajili ya mchanga wa madini!
 
Ni watuhumiwa walioficha magari wakidai ni mitumba wamefikishwa mahakama ya Kisutu, habari hii nimeileta kwa kuwa kulikuwa na kuaminishwa kuwa hakuna waliokamatwa kwa kuficha Magari bali ni kiki ya kufunika habari za Nape

Nashangaa kwa nini imekuwa sifa kusema uongo? Rais, alisikika ikwapongeza watumishi wa bandari kwa kutumia vizuri scaner kubaini magari kwenye container za mitumba. Kutokana na maelezo ya Mhe. Tundu Lissu ni kwamba watuhumiwa wamekaa kituo cha polisi bandari bila kufikishwa mahakamni au kupatiwa dhamana kwa muda mrefu. Ina maana watuhumiwa walikamatwa hata kabla ya Mheshimiwa Rais hajaenda! Aliyegundua ni Mhe. Rais au watumishi wa bandari na rais alioneshwa tu? Kwanini sifa ziende kwa rais katika suala hili? Kuna dhambi gani kuwasifia waliotenda kazi? Haya yanatia shaka dhamira zetu.
 
Wamelazimika kuwafikisha mahakamani baada ya makelele ya wadau kuwa wamekaa mahabusu kwa wiki tatu bila dhamana na bila kufikishwa mahakamani! Ni aibu!
 
Ni watuhumiwa walioficha magari wakidai ni mitumba wamefikishwa mahakama ya Kisutu, habari hii nimeileta kwa kuwa kulikuwa na kuaminishwa kuwa hakuna waliokamatwa kwa kuficha Magari bali ni kiki ya kufunika habari za Nape

Siku nyingine usiwe unaleta habari za kutaka kupotosha umma kwa kumtafutia mtu kick kwa ulazima. Msilazimishe mambo jamani.
 
mods, title ya hii thread ni totally misleading.

JPM hakudaka mtu yeyote wala makontena bandarini bali alionyeshwa na watu wa TRA na TPA makontena yaliyokwisha kudakwa tayari.

hata yale makontena ya concentrates (mchanga) hakuyadaka wala kuyazuia siku ile. yalikuwepo pale kitambo baada ya kupitia taratibu zote za kawaida kisheria isipokuwa yalikuwa yamehifadhiwa bandarini kusubiri plight yake baada ya zuio la kutoku-export concentrates rais alilolitoa wiki kadhaa kabla ya ziara hii ya sasa bandarini.

it's extremely annoying kuona waganga njaa wa Lumumba st wana-distort facts na watu wanameza tu bila ku-digest. it's even more annoying kwa hata mods wa JF, wahariri wa media houses, etc now kuingizwa blindly kwenye hii propaganda bandwagon. sickening!!
 
Hawa walishikwa na TPA toka siku nyingi..

Siku ile JPM ameenda port hawa jamaa tayari walikuwa tayari wana zaidi ya wiki pale kwenye selo za polisi bandari...

Acha kupotosha kwamba walidakwa na JPM...

JPM yeye alikuwa anapewa taarifa ya hili tukio lakini watuhumiwa walikuwa ndani tayari.

Kwa hiyo JPM kaiga tabia za Kamanda Kova kutoa Silaha store na kutangaza kazikamata huku kavaa Gloves!
 
Mtoa mada mbona haikutangwazwa walipokamatwa,hizo kiki zenu mziache,na watatoka kwa dhamana,na hakuna kitakachoendelea.
 
Back
Top Bottom