Walinzi Watatu wa Suma JKT Watiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Kompyuta 50 Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM

SON2016

Member
Jan 3, 2016
64
37
Walinzi watatu wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Dodoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa kufikia 50 mali ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa wizi huo ulitokea juzi baada ya chuo hicho kufungwa kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.

Inadaiwa kuwa katika wizi huo baadhi ya walinzi wa Suma JKT ambao wanajukumu la kulinda chuo hicho, walihusika huku watatu wakishikiliwa na polisi.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa baadhi ya askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma wanadaiwa kuhusika na kuzua mkanganyiko katika uchunguzi wa tukio hilo.

“Katika wizi huo, pia kuna askari kutoka mjini ametajwa na walinzi wa Suma JKT kuhusika, sasa baada ya kupata taarifa hizo ndiyo wanafanya mpango wa kumkamata,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Ofisa Habari wa Udom, Beatrice Baltazar jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba, bado hawajajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibiwa.

“Ni kweli kuna wizi wa kompyuta hapa chuoni, lakini sijajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibwa, ila kuna walinzi watatu wa Suma JKT wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano,” alisema Beatrice.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa naye alithibitisha kuwapo kwa taarifa za tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa kuwa yupo likizo.

Hata hivyo, Mambosasa alikanusha kuwa hakuna polisi aliyehusika katika tukio hilo bali ni walinzi wa Suma JKT.

“Hakuna askari wetu aliyehusika katika tukio hilo, wenye jukumu la kulinda chuo hicho ni Suma JKT ndiyo wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mambosasa.
 
Chuo kikubwa kama UDOM kinaibiwaje computer nyingi kiasi hiki.. hakuna CCTV camera za kusaidia ulinzi wa mali zenye thamani kubwa kiasi hiki..? Ni mambo ya aibu.
 
Hao watu ni shida kwenye administ.hawawezi kabisa,we chuo kikubwa hakina maji,wanafunzi wanapata shida ,hasa vyooni,hata visima hawana ,bora wastaafu,ni mara mia.mkachukua mtu anaeweza uongozi mkalipa kiasi kikubwa lakini maendeleo yanaonekana,
 
Mkuu naona umeanza KUTUMBUA JIBU. Embu jisogeze zaidi
 
Mkuu naona umeanza KUTUMBUA JIBU. Embu jisogeze zaidi
Yap nasubiria bunge tuwalipue,wanafunzi wamefungua chuo.mwezi.wa 11 hawana maji,masewage system yanafurika balaa,yaani km hawapo maofisini,ila wenzetu hawa kwenye uongozi hawawezi kabisa,vyoo vichafu,maji ya kunaw macanteen ni shida,wakati ddm maji yamejaa,tunapowaambia watu mtaani wanashangaa
 
Chuo kikubwa kama UDOM kinaibiwaje computer nyingi kiasi hiki.. hakuna CCTV camera za kusaidia ulinzi wa mali zenye thamani kubwa kiasi hiki..? Ni mambo ya aibu.
Hata maji hamna ndo wawaze cctv ,wamerogwa ni nini,sidhani km hata wanazifahamu hao maprofesa ,wana akili za kiacademic tu,za uongozi hawawezi kabisa,
 
Yap nasubiria bunge tuwalipue,wanafunzi wamefungua chuo.mwezi.wa 11 hawana maji,masewage system yanafurika balaa,yaani km hawapo maofisini,ila wenzetu hawa kwenye uongozi hawawezi kabisa,vyoo vichafu,maji ya kunaw macanteen ni shida,wakati ddm maji yamejaa,tunapowaambia watu mtaani wanashangaa
Na mimi nilishangaa nilipoambiwa na mwanangu kuwa maji ni shida wanaoga kwa zamu
 
Hao watu ni shida kwenye administ.hawawezi kabisa,we chuo kikubwa hakina maji,wanafunzi wanapata shida ,hasa vyooni,hata visima hawana ,bora wastaafu,ni mara mia.mkachukua mtu anaeweza uongozi mkalipa kiasi kikubwa lakini maendeleo yanaonekana,
Umezungumziwa wizi wa computer hayo mengine weka uzi wako watu wachangie usitutoe kwenye mada.
 
Back
Top Bottom