Mshahara Mdogo!Unatia uvivu kufundisha na mbaya zaidi unasikia wapuuzi fulani wako bungeni wanakula hela ya kutosha bila kutumia nguvuHabari wana jukwaa.
Hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa walimu hasa wa shule za msingi kuwarekodi watoto na kisha kuzisambaza video hizo,
Binafsi nimefanikiwa kuona video 3 za walimu hao na zote zinaonesha si tu uelewa mdogo wa mwanafunzi bali pia ujinga wa aliyepewa dhamana ya kuuondoa ujinga wa mwingine.
Mwalimu anamuuliza mtoto kwanini hakuja shule? Mtoto anajabu hakuja kwa sababu alifariki. Kiswahili anachotumia mwalimu huyo na majibu ya mwanafunzi inaonesha kuna tatizo kubwa katika jamii.
Cha kujiuliza ni nini kinapelekea mtu kumrekodi mtu aliyepewa dhamana ya kumvusha toka alipo, halafu anamsambaza mitandaoni. Au ni stress za udogo wa mishahara?
Mwalimi akijichanganya akafanya huo upuuzi kwa mdogo wangu atahama mji la sivyo atapata tabu sana.Hongera sana kwa walimu wanaofanya hivyo serikali inapaswa kujiongeza
akikujibu ni tagooo...Umekuja na ushahidi gani kuthibitisha kwamba hao ni walimu na sio waigizaji ama wahuni tu!?
si kweli! analysis yako ipo chini sana ya kiwango endelea kufanya utafiti wako upya mkuuMwalimu kusambaza video za namna hiyo ni moja ya madhara ya kuchukua wanafunzi waliopata madaraja ya chini katika matokeo ya kidato cha 5 na 6 ndo wakasomee kozi ya ualimu. Mtu mwenye uelewe mzuri hawezi kufanya kitendo cha namna hiyo.