Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Walimu wakuu 21 wa shule za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wamevuliwa madaraka kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ya fedha kwa kuruhusu usajili wa wanafunzi hewa pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe,Frank Bahati amesema amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya walimu hao kushindwa kuwajibika ipasavyo na kukosa umakini katika usimamizi wa maendeleo ya shule,ikiwemo taaluma na miradi ya shule pamoja na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.
Amedai kuwa uzembe wa walimu wakuu hao,pia umesababisha shule tano za msingi wilayani humo kufungwa kwa kukosa vyoo,baada ya walimu hao kushindwa kutekeleza agizo lake la kuwasilisha mpango mkakati wa kutatua baadhi ya changamoto katika shule zao ikiwemo ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa.
Halmashauri ya wilaya ya ukerewe inayoundwa na jumla ya visiwa 38 ina shule za msingi za serikali 123,walimu 1600 na wanafunzi 102,114.
Chanzo: ITV