Walimu wagoma, kisa mwenzao kuzabwa kofi darasani

White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
1,034
1,165
WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.

Makamu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Kipesha alisema wameitisha mgomo huo wa siku mbili kupinga kitendo cha Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao Jacob Msengezi (25) ambaye anafundisha somo la Hisabati Darasa la Saba shuleni hapo.

“Licha ya kulaani vikali kitendo hiki cha udhalilishaji alichofanyiwa mwalimu mwenzetu na Ofisa Elimu (DEO) wetu (Peter Fusi) kumcharaza makofi mbele ya wanafunzi wake akiwa darasani ….

Ametudhalilisha sote yaani hata hamasa ya kufundisha imetoweka ….. “Sasa hatutaingia darasani kufundisha kwa siku mbili tukimshinikiza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Adam Missana) achukue hatua dhidi ya ofisa huyo wa elimu ……yaani tunadhalilishwa hivi mbele ya wanafunzi wetu wenyewe wakati kazi hii tumeisomea na tuna vyeti halali ….

Tukiwa na sifa stahiki za taaluma ya ualimu,” alieleza Kipesha. Akifafanua, alisema walimu hawataingia kufundisha kwa siku hizo mbili na watakuwa ofisini wakiandaa mitihani huku wanafunzi wakiendelea kuhudhuria shuleni hapo kama kawaida.

Naye Mwalimu Msengezi alilieleza gazeti hili kwa njia ya simu akiwa shuleni Kianda kuwa juzi Jumatano Ofisa Elimu, x alitembelea shuleni hapo saa tatu asubuhi akikagua mazingira ya shule.

“Mie wakati huo nilikuwa darasani na wanafunzi wa darasa la saba nikisahihisha madaftari yao kwani tayari kipindi changu kilianza saa 2:00 na kumalizika 2:40 asubuhi … Hivyo kwa kuwa mwalimu wa somo la Kiingereza alikuwa ‘busy’ akitunga mitihani niliamua niutumie muda huo kubaki darasani humo nikisahihisha madaftari,” alieleza Msengezi Kwa upande wake, Katibu wa CWT Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Vicent Ndewele akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kuwa chama hicho kitatoa msimamo wake leo.

Source: mpekuzihuru
 
Huyo hana sifa ya kuwa Afisa Elimu.Hivyo mkurugenzi atumbue tu hilo jipu,hajui taratibu za kazi.sasa huko ofisini si anafanya madudu kabisa.
 
Stupid , ushahidi wa kutosha mnao, mpeleke mahakamani!
 
inasikitisha sana kuwaonea walimu maana mazingira ya kazi ni magumu sana..kwanza isitoshe waliofaulu hesabu ni wengi na wanaojua hesabu ni wengi pia ila mazingira magumu ndio maana wengi hawataki kufundisha sasa waliojitolea nao mnawapiga sio haki hata kidogo...
 
Nilikataa kwenda huko peripheral kwa sababu kama hizi. Ningepata kesi ... Huwa sipendi kuonewa, ningejibu mapigo aisee! Dadeki.

Huku mjini hakuna upuuzi wa kuonewa hivyo kwa mfanyakazi wa umma. Kuna namna nyingine ya kunionea, sio hiyo ya kunipiga kofi aisee.
 
Huyo mwalimu ni mdhaifu tu, ingekuwa mimi timbwi lake hapo ingebidi waje FFU kuamulia tena na mabomu, shule ingefungwa automatically sio kwa mgomo
Mpaka FFU wafike wallah atakuwa amechafuka! Hata kama atakuwa bouncer namna gani lazima akae! Nyama kitu gani bwana hata kwenye sambusa si kuna nyama?!! Hiki ki-mwalimu nimejupuuza sana, hata kama atakuwa Mzee alistahili kuwa na busara hawezi kumpiga makofi mwalimu mbele ya wanafunzi!
 
Naomba nikukumbushe, mimi ndiyo baba yako hivyo unamtukana baba yako. Huyo mama yako aliekuonyesha ni wa kufikia. Nakupa siri hiyo, tulikuzaa kabla ya huyo wa kufikia . Umepata laana maana umemtukana baba yako. Muulize mama yako baba ni nani atakwambia Chuakachara

hahahahaaaa lazima jamaa awe mpole
 
Ni kazi ngumu sana halafu sumbawanga haifatiliwi sijui ipo mwisho wa Tz sanaaa!
Na nyie white party ni wadhaifu mno wacha mzabwe vibao labda mtazinduka! Mlimwachaje akatoka mzima huyo mwehu? Halafu eti mnagoma huku mnakaa ofisini kutunga mitihani? Mgomo gani huo? Pia elewa shule ya Msingi hatuna makamu mwalimu Mkuu bali tuna mwalimu Mkuu msaidizi!
 
Tunataka viongozi kama huyu Afisa Elimu....kwa ajili ya Tanzania mpya......
 
Back
Top Bottom