Walimu wacharazwa mapanga wakiwa njiani mkoani Mara

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,659
2,822
Taarifa zinasema kuwa watu waliofanya tukio hilo bado hawakuweza kufamika mara moja ambapo mmoja ya walimu aliofanyiwa unyama huo alieleza kuwa suala hilo limekuwa likijitokeza mara nyingi.

Walimu watatu wa shule ya Secondary Mara iliyopo katika manispaa ya mji wa Musoma Mkoani Mara,Vedastus Rwechungula, Juma Amos Na Maccelo Ndege, Wamekatwa Mapanga sehemu mbali mbali ya miili yao walipokuwa wakirejea shuleni hapo Usiku wa Saa Nne toka matembezini.

Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Musoma,Walimu hao wamesema kuwa Vitendo vya Uhalifu jirani na Shule hiyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kutokana na vibaka waliopo katika eneo hilo kuwakata watu kwa mapanga.

Chanzo: Swahili Media
 
Pole sana walimu, Mwenyezi Mungu atawasaidia mpone haraka. Kwa kweli kazi ya ualimu ina changamoto sana
 
Huwa najiuliza hawa wakurya mbona wakiwa mikoa mingine wanakuwa wapole mno ni nini huwapata wawapo kwao...Ama wanaogopana kuchukiliana sheria? Polen walimu.
 
Ukiwa pande za ukuryani jihadhari sana na mambo ya kutamani mademu za watu na mashauzi ya kujifanya unatoatoa ofa za bia jifunze kuyasahau.
 
Taarifa zinasema kuwa watu waliofanya tukio hilo bado hawakuweza kufamika mara moja ambapo mmoja ya walimu aliofanyiwa unyama huo alieleza kuwa suala hilo limekuwa likijitokeza mara nyingi.

Walimu watatu wa shule ya Secondary Mara iliyopo katika manispaa ya mji wa Musoma Mkoani Mara,Vedastus Rwechungula, Juma Amos Na Maccelo Ndege, Wamekatwa Mapanga sehemu mbali mbali ya miili yao walipokuwa wakirejea shuleni hapo Usiku wa Saa Nne toka matembezini.

Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Musoma,Walimu hao wamesema kuwa Vitendo vya Uhalifu jirani na Shule hiyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kutokana na vibaka waliopo katika eneo hilo kuwakata watu kwa mapanga.

Chanzo: Swahili Media
Na bado wanaenda kula bata hadi usiku.....ni sawa na kukatiza bonde la mkwajuni au jangwani saa sita usiku.
 
Wakurya niwatu wema sana lkn sijui baadhi yao wanamatatizo na ujasiri ulopitiliza ndomaana wanafanya mambo hayo... Vilevile yapasa mjue Mara ni mkoa wenye makabira ya ASIRI mengi TZ nzima na Afrika nzima pengine hata dunia nzima KWA MUJIBU WA TAFITI ZILIZOPO kwaiyo yapo makabira mengine wanaoweza kufanya vitendo kama ivyo lkn kwakuwa mkurya ndo keshkaliliwa basi atabebeshwa mzigo huo... Kunya anye kuku akinya bata basi kaharisha
 
Ukiwa pande za ukuryani jihadhari sana na mambo ya kutamani mademu za watu na mashauzi ya kujifanya unatoatoa ofa za bia jifunze kuyasahau.
Asante sana mkuu. Nilikuwa nataka kutoa angalizo Hilo pia. Kwa mujibu wa utaalamu wangu wa haya matukio asilimia 80 huwa yanahusu mambo ya wanawake au wake za watu. Mara hakuna matukio ya kipuuzi kwa sababu watu hawana mchezo kule. Wakitambua unajihusisha na upuuzi wa kukaba watu hata baba yako mzazi anaweza kukuchongea Raia Wakaja kuchukua sheria mkononi. Kwa hiyo kwa ufupi watu wa Mara huwa tunaheshimiana sana. Hawa wageni wanavamia wake na mademu za watu ndio huwa yanawakuta.
 
Back
Top Bottom