Kilosaone
JF-Expert Member
- May 3, 2015
- 411
- 224
Adui wa mwalimu ni mwalimu
Mwalimu ndiye alikuwa kiongozi wa nchi ya Tanzania tofauti na marais wengine wa Malaysia, South Korea, Taiwani, Singapore ambao walitawala kipindi kimoja na Mwalimu. Bahati mbaya nchi hizi zilikuwa nyuma kiuchumi na zilizokuwa zimegawanyika kimakabila na ukanda.
Fursa adhimu nchi hizi viongozi wake waliboresha mtizamo wao dhidi ya mwalimu. Walimu katika nchi mfano Korea ya Kusini hupewa kila kitu ikiwa ni posho ya familia na kusomeshwa watoto wa mwalimu hadi chuo kikuu bure na serikali yaani mwalimu huachwa awaze namna ya kujenga fikra (building education) za wananchi.
Njoo kwetu muasisi wa nchi alimuona mwalimu kama mtu anayestahili kujitolea na kazi yake haina maana kiasi cha kumuacha mwalimu akisononeka kwa uwingi wa majukumu, yaani hadi leo usishangae mwalimu anagombana na wanafunzi kisa hawajanunua ubuyu kwake. Wanaume kutwa na bodaboda, mikopo kila kona yaani huyu mwalimu atujengee watoto wetu ili baadae wawe wabunifu na viongozi bora.
Mjomba mimi naona umejitahidi kununua ndege nyingi kwa maendeleo ya nchi ila uliowakabidhi hawakuandaliwa vizuri wanajua tumbo na ndugu zao ndiyo kila kitu si taifa. Viwanda itakuwa ndoto kwani mwalimu aliyechanganyikiwa zao lake ni waliochanganyikiwa.
Nawasilisha
(NIMEKOPI TOKA GROUP LA WALIMU FACEBOOK)