Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mwezi uliopita katika maeneo ya posta ya zamani,karibu na forodhani primary school, begi la fedha lilianguka kwa bahati mbaya kutoka kwenye gari iliyokuwa inakatiza. Rundo kubwa la vijana waliibuka barabarani na kuzigombea noti nyingi nyekundu.
Wengine walitoka nyuma ya zile ofisi za kukatia tiketi za boti ziendazo Zanzibar, wengine walitokea karibu na posta ya zamani, wengine walitokea kwenye ile bustani iliyopo mbele ya NBC, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika. Hakuna aliyejali magari yaliyokuwa yakikatiza mida ya saa saba mchana, na ni bahati kwamba madereva wa Dar walikuwa wastaarabu, walipunguza mwendo ili vijana wazipambanie noti za bure, wagombee neema iliyowaibukia bila ya kutegemea.
Mwenye nguvu ndiye aliyekula nyama, wale wenye misuli kama mabaunsa waliambua noti nyekundu zaidi ya kumi, wale wembamba waliambulia noti moja. Kitu cha kusikitisha, kwa jinsi nilivyowaona vijana wake, umri wao ni kati ya 18-35. Umri sahihi katika uzalishaji, lakini ubangaizaji ndio unawaweka jijini.
Rais JPM anaposema watu wakalime kwa nguvu ni kwamba anawaongelea aina hiiya vijana. Lakini mimi nadhani kinachotakiwa kufanyika ni kuleta mapinduzi kwenye elimu ya VETA. Kitu cha pili ni kuhakikisha mapitio ya sera ya michezo yanafanyika katika hali ya umakini. Kwani michezo inao uwezo mkubwa wa kuajiri kundi kubwa sana la vijana.
Didier Drogba katika hospitali yake, ameajiri madaktari ambao wanaendesha maisha yao na ya wale watu waliowaajiri majumbani mwao na kwenye miradi yao binafsi.
Maria Mutola mwanariadha wa zamani wa Msumbiji anaendesha taasisi yake huko kwao, anawatengeneza vijana waweze kuwa wakimbiaji kama yeye, kaajiri watu wengi kwenye miradi yake.
Wanariadha wa Ethiopia na Kenya wanaobeba medali kwenye olimpiki, wanategemewa na jamii zao na wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na tatizo la ajira.
Kuwapeleka vijana kwa nguvu kwenda kulima, isiwe ndio suluhisho la mwisho. Yanahitajika mapinduzi kwenye utoaji wa elimu ya ufundi (VETA) pamoja na mapinduzi ya michezo. Mdogo mdogo ipo siku tutafika.