Wale waliofukuzwa na wengine kuhamishwa Tambaza Secondary 1993 mko wapi?

Washkaji wote waliosoma tambaza enzi zileeee big up sana, mnamkumbuka nyau, Mwl. Mushi, LIle sooo la Kuwatwanga Jitegemee sec, Kakonda kalidanji mitaa ya Keko, Mnakumbuka ile mikanda uliyokua unachapwa pale kantin kugomea menyu? Kina Dictetor mpoo? Kina Kanaluza.

Lile soo la vitabu ni soo babaake, kuna mtu ambaye alikosa volume siku ile kweli?

Usidanganye watu, Jitegemee waliwatoa Tambaza mkuku uwanja wa taifa na kipondo KIKALI hasa tukisaidiwa na Jeshi hasa mlivyofungwa kwenye fainali ya UMISETA, kimbizwa mpaka mitaa ya Maduka mawiwli na Keko , Wakeenda mitaa ya shule ya uhuru na kumpiga na kumwua Konda wa daladala kumalizia hasira zao
Mkuu wa Jitegemee akachonga jalada kwa Wizara ya Elimu la kuwamaliza Tambaza na wakaandaliwa wanafunzi kama, usahahidi na wakapelekwa kufanya utambulisho hewa, wanakawa wanaonya tu kidole huyo na huyo. Kesi ikawa kubwa, hapo ndio mwisho wa Tambaza O level.
 
Naikumbuka hii Mwana, walipita wadada warembo na wakaka kupoint watu, mie waliniacha. Nilikua nimevimba mkono wa kulia nilipigwa gongo na mwanajeshi katika kukimbizana ile siku kwenye viunga vya uwanja wa uhuru enzi hizo. Ile siku ilikua balaa sana. nilitembea kwa miguu hadi Buguruni...... Ila kwenye ile mechi Jitegemee mlikua mnabebwa sana. na chanzo cha vurugu....
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia kulikuwa na "ugomvi wa jadi" kati ya Azania na Tambaza mpaka hili suala likaongelewa Bungeni, maana kwa kweli hali ilikuwa mbaya
Yeah, enzi za Andrew Kwayu - Head Master wa Azania. Ugomvi ulikuwa sana sana kwa madogo ya O-level.
 
Naikumbuka hii Mwana, walipita wadada warembo na wakaka kupoint watu, mie waliniacha. Nilikua nimevimba mkono wa kulia nilipigwa gongo na mwanajeshi katika kukimbizana ile siku kwenye viunga vya uwanja wa uhuru enzi hizo. Ile siku ilikua balaa sana. nilitembea kwa miguu hadi Buguruni...... Ila kwenye ile mechi Jitegemee mlikua mnabebwa sana. na chanzo cha vurugu....

Yaani nakumbuka kama inabidi ushukie kariakoo kuunganisha uende home lazima tunakuwa tunatembea kama kumi, Tambaza walikuwa Wanasubiri Jitegemee mitaa ya Shule ya uhuru
Kwenye mechi baada ya vurugu Tambaza wote wakatoka uwanjani tukajua wanaenda zao, kumbe wameenda kukusanya mawee, sisi tukawa tunasherekea mara tulianza kuona mawe yanavuka ukuta yanaingia uwanjani kama mvua, duuh watu kibao waliumia, sasa Wajeshi wakatukusanya kama kikosi na kuamuru shambulia, wote tukaanza kelekea getini, ile kufungua tu tulikutana na mawe ya kutosha, tukafunga geti tukakusanya mawe yote yaliyoingia , tukafungua geti baada yapo ni historia mpaka tulianza kuwasaidia wanafunzi wa tambaza waliowekwa mtu kati , tunawanyofoa tuwaambia kimbia hasa,
tukawafuata mpaka maduka mawili, kesho yake ndio taarifa za kifo cha konda

Tambaza walikuwa wanawaonea sana Azania, Mzizima na Shabaan Robert lakini kiboko walikuwa kinondoni muslim walikuwa wababe wa tambaza na Jitegemee tukasema hapa watatosha wakiingia anga
 
Wanafunzi wa miaka hiyo inaonekana baadhi walikuwa vichwa vibovu sana,ila pamoja na ukorofi wao kuna vitu walivi-gain kwenye maisha yao siyo wanafunzi wa kileo kuvaa tusuruali twa kubana na ndala na soksi miguuni akili zimelala zaidi ya samaki pono.

Sijui watahadithia nini vizazi vyao kama hapa.
 
Hamna lolote, nyie Jiteute mlisaidiwa na JWTZ, MP kibao ndio waliotukimbiza ile siku. Hata sababu ya Tambaza kusambalatishwa ni ugomvi wa Azania na Tambaza, Chanzo kikiwa demu wa Zanaki, sio na Jitegemee.
 
Daah! Umenikumbusha mbali sana unapolitaja hili daladala simba luwala. Nadhani lilikuwa ubungo kariakoo au posta. Ilikuwa miaka ya 1985 na kuendelee. Nakumbuka mechi zilizokuwa zinachezwa pugu sec. Ilikuwa kazi kubwa azania inapocheza na tambaza au tambaza na kinondoni. Bakora na ngumi nje nje. pamoja na fujo zote lakini shule zilikuwa na wanafunzi vichwa na tulikuwa tunajuana nani bingwa wa maths, physics, kemia na biology miongoni mwa wanafunzi wa shule hizo. Namkumbuka Benedict ndomba wa tambaza miaka ya 1984- 1987, modest stanley chindonga azania 1984-1987. wana njawa azania(84-87) Modest ni mhandisi tanesco ila sikui Benedict yupo wapi
Du umenikumbusha mbali ,enzo hizo niko Jangwani Sec
 
Wanafunzi wa miaka hiyo inaonekana baadhi walikuwa vichwa vibovu sana,ila pamoja na ukorofi wao kuna vitu walivi-gain kwenye maisha yao siyo wanafunzi wa kileo kuvaa tusuruali twa kubana na ndala na soksi miguuni akili zimelala zaidi ya samaki pono.

Sijui watahadithia nini vizazi vyao kama hapa.
Sana yaan. wanafunzi wa siku hizi maboya sana.
 
Wakati O level bado ipo Tambaza, ambapo ilikiwa ya wavulana watupu, A level ilikuwa na waschana wachache sana.

Sitasahau kundi la Wu-Tamba, walikuwa wanamchokoza sana rafiki yangu Isabela(RIP).
 
Ilikuwa Shule ya ndoto yangu kwa “A” level,
Na nikajaliwa kuchaguliwa,
Nilifirahi sana

Yani nilipokuwa nikiwaona uniforms zao za wanafunzi wa kike wanavyovaa viatu vyeusi na soksi nyeusi na rangi ya skirts zao zilinivutia sana Yani ilikuwa kama askari wa Kike (WP).

Yani hakika nilifirahia sana TAMBAZA (Tazama Mbali Zaidi).
 
Hamna lolote, nyie Jiteute mlisaidiwa na JWTZ, MP kibao ndio waliotukimbiza ile siku. Hata sababu ya Tambaza kusambalatishwa ni ugomvi wa Azania na Tambaza, Chanzo kikiwa demu wa Zanaki, sio na Jitegemee.

Tambaza walikuwa wanonekana wajanja sababu shule ya Tambaza ilikuwa maeneo ya watoto wa mama UPANGA, mlikuwa mnawatesa Azania , Shaban Robert Na Mzizima tu
Mkienda mechi shule za uswahilini mlikuwa kama mmemwagiwa maji, hata Kibasila mlikuwa hamuwawezi, mkienda maeneo ya Kinondoni ndio kabisa hata mechi hamuendi kushangilia timu yenu,
Hiyo stori sijui ya demu wa Zanaki haihusu ilikuwa nyongeza kwenye kesi kuu ya mlibambikiwa na Jitegemee.
Mlikuwa na fujo za kitoto Don Bosco miaka hiyo hasa hasa na Azania tu sababu mashindano ya Don Bosco kulikuwa na timu za uswahilini Migomigo na Kinondoni,
 
Ilikuwa raha sana miaka hiyo, The Golden 90s , OPP, NWA, PUBLIC ENEMY, EPMD, HEAVY D, kwetu bongo Walikuwa KWANZA UNIT na RIP Nigga One enzi hizo DJ BONNIE LOVE hakosi kila Graduation ya Form 4,
Mitumba ndio fashio kali zinapatikana, Jeans na Raba za kuparama na kuchumpa, lakini usiku, muuza mitumba anapendeza nazo disco, anakwambia naziajasti tu, asubuhu anazitundika mtaa wa congo,
Maeneo ya Temeke ni mchiriku kwa kwenda mbele, watoto wa Upanga wote mabaunsa, Safari ya karibu ilikuwa South Africa , watoto wa shule wanaiba kwao Video Decki (VHS), bei kilo tatu , akiuza anapotelea South,
na wajanja wote ilikuwa akili ni SAFARI,na lakini sio wengi kuzamia , wengine tu waliondoka kitaaluma na kupotelea mbele kwa mbele , kwenda UK ilikuwa VIZA FREE, wewe tu na nauli yako.
 
Hivi nini kilitokea hadi hiyo VISA free to UK ikatolewa!??
 
Nchi nyingi za Common Wealth Member zilikuwa Visa Free miaka hiyo, Uganda , Kenya , Zambia na Zimbabawe na nyinginezo
Nchi nyingi na Tanzania zilibaniwa sababu ya zillikuwa zinatumiwa na watu wa nchi nyingine ambao walipigwa ban siku nyingi walikuwa wanatumia passport zao kusafiri.
Miaka hiyo passiport imebandikwa picha ya studio, wajanja wanatoa kiulaini wabandika ya kwao.
 
Sie tuliosoma A-level na wasichana ngoja tuangalie maisha ya wakongwe kabla yetu
Kabisa mkuu ,wakati nasoma A_level siku moja njiani wakati naelekea stendi kuchukua gari kwenda skuli nilikutana na mmoja wao wa kizazi cha wakorofi naye akielekea stendi kupata usafiri alinijua kwa kuona sare ,basi akajitambulisha na kuanza kunisimulia mikasa na vituko walivyofanya alisema wengi wao walishindwa kuendelea zaidi ambao wazazi hawakuwa uwezo kutokana na kutupwa shule za mbali ,nilisikitika sana wengine hawakuhusika na wafuata mkumbo kuangamia kwa mambo ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom