Wale wa punda kusukuma mkokoteni mmeona pia inawezekana mkokoteni unaweza kumkokota punda

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Ni nadra kwa mkokoteni kumkokota punda lakini kwa utawala huu wa Rais Magufuli tumeona akitumia mbinu ya mkokoteni kukokota punda pale punda anapoonekana dhaifu au hataki kukokota mkokoteni. Takribani mwezi mmoja uliopita, kuna mjadala uliojitokeza uliokuwa unasema ‘ili mzigo/ mkokoteni ufike ni budi punda akokote mkokoteni’. Ni mjadala ulioibuka baada ya serikali kusitisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambao ulitazamiwa mapema kabla ya miradi mingine hasa SGR.

Watu walioanzisha mjadala huo waliufananisha mradi wa bagamoyo kama punda na miradi mingine kama SGR ni mkokoteni hivyo ili mkokoteni uende ni lazima punda aukokote. Walioanzisha mradi huo hawakujua punda yule ni dhaifu na goigoi na hawezi hata kujisukuma mwenyewe sembuse kusukuma mkokoteni. Punda yule alitaka kulishwa chakula cha gharama ambacho bosi wake anakila na akasahau hata mahukumu yake ni kukokota mkokoteni w bosi ufike.

Bosi huyo ni mjanja sana, alifunga mota kwenye mkokoteni inayojiwasha automatiki pale punda anapochoka na kushindwa kukokota mkokoteni ili mkokoteni umkokote punda. Na tumeshuhudia hekima hiyo ya bosi imetusaidia mkokoteni kumkokota punda mwenye majivuno na asiye na fadhila. Yupo wapi punda yule aliyejiona sawa na bosi wake? Hakika punda huyo anataabika kwa kukosa mtu wa kumuhudumia kwa chakula na malazi, yupo kajichokea anasubiri kufa sasa.

Leo utawala wako umetuachia falsafa pana hasa kuona mateke ndo fadhila za punda, na Zaidi ni kutusaidia kujua kuwa punda aliyedhoofu na asiye na shukrani usimtegemee sana kukufikishia mkokoteni wako badala yake tumia njia ya kufunga mota automatiki itakayoweza kukokota mkokoteni pindi punda akijiona ana hadhi sawa na bosi wake. Hongera kwa hii falsafa nzuri mhe.Rais
 
Hahaha hahahahaah umeeleweka mkuu ila yule bingwa anapingana na boss wake
 
Bado tu hujapata uteuzi ,unahangaika kweli na mada zako za kichwa chini miguu juu ,uweke namba za simu na anuani kamili kuwahisha uteuzi ,usipoweka unajichelewesha mwenyewe .
 
Punda wetu alipitia china wakamlisha power point akasadiki ,
Mikokoteni ikaanza kumvuta akarudi nchini na mawazo ya mikokoteni kua wanafadhili 100/100 kwann serkali inawapiga pini
 
Bado tu hujapata uteuzi ,unahangaika kweli na mada zako za kichwa chini miguu juu ,uweke namba za simu na anuani kamili kuwahisha uteuzi ,usipoweka unajichelewesha mwenyewe .
pole kama nimegusa maslahi yako au ya mtu wako. unateseka sana na pingapinga na hii ni moja ya ishara ya mateso wanayopata watu kama ninyi wanaposikia JPM akitajwa
 
Back
Top Bottom