Wale funza wa miguu waliishia wapi?

Niseme tu wazi wengi tuliozaliwa kidogo 90 kurudi nyuma, 80, 70 aisee hii nchi imetutesa sana, ufukara ulikuwa wa kiwango cha juu sana, ukianza uvaaji wa viatu shida, chupi za VP, mafuta yalikuwa petroleum jelly tu, yani zao la kutoka ktk bidhaa ya petrol, ustaarabu ulikuwa bado sana, usafiri shida ile mbaya kabisa.

Watu walikuwa wanavuta sigara kama fashion, iwe kwenye basi, mgahawani au popote pale akiona watu anawasha manake ni fashion.

Viatu shida, kama ukipata sana unakuwa na araiyoo au ng'inyira, familia yenu ikiwa safi basi unapata chachacha, au kama wa kike utapata loso, zikaja zico n.k

Usafiri full tabu, basi likipita sahau lingine mpaka kesho yake, idadi ya waliosimama ni wengi kuliko walio na siti, mwaka 89 niliwahi safiri toka moshi mjini mpaka iringa mjini nikiwa nimesimama, basi la kampuni ya comfort la mchaga wa marangu, plate number MSB......

Yani mzee mkapa ashukuriwe mno na asamehewe madhambi yake.

Funza kuwa nazo haikuwa aibu manake ilikuwa kampeni mpaka mashuleni kutoana.
 
Watu wengi sana hawajui kuwa hawa funza (jiggers) wanatokana na viroboto (flea). Kwa hiyo ukisema funza wamepotea ina maana viroboto siku hizi hakuna.

Kuenea kwa funza miguuni mara nyingi ni suala la uzembe tu. Hii hapa chi labda ni worst case ya kuwa na funza

 
Upatikanaji wa maji ndio umekomesha hao funza, maeneo yenye maji huw hao wadudu hawazalianz na hufa
 
Watu wa zaman usafi mlikuwa hamtilii mkazo lakin pia issue ya afya na chanjo hazikuwa zinapatikana.

Kifupi maisha yameimarika sana kwa sasa.
 
nishawah pata mara moja aseee,ila kale ka muwasho n fantastic 😂🙌🏾
 
ni kweli uchumi ulikuwa mbaya. ni matokeo ya vita ya amin. marehemu mzee ruksa na mkapa walifanya makubwa sana kuifungua nchi na kuitoa nchi kwenye maisha ya ujima ya kuwasha vijinga vya moto na vibatari (hiki kibatari najua kuna wengi tu humu wasiokijua nitakielezea siku moja kilikuwaje na jinsi kilivyofanya kazi[emoji1])
 
uko sawa mkuu funza ni zao la viroboto km wale wanaoonekana kwa mbwa au kuku. lakini hawa walikuwa spesho maana walikuwa na uwezo wa kuingia ndani ya ngozi laini ya binadamu na kuzaliana humo.
 
Kati ya viumbe walio hatarini kutoweka wanahitaji kulindwa kwa sasa
 
Mabasi yameandikwa kabisa "USITEME MATE NDANI"
 
Nakumbuka kuna kipindi nikiwa secondary tulienda kibosho aisee tulimkuta binamu yangu ana funza wengi jamani mpaka hawezi kutembea vizuri.Tukamshika(alikua mdogo kwangu) na kuanza kumtoa.
 
Mabadiliko mengi yameanzia kwa mzee Ruksa msijisahaulishe.
 
Kama ushawahi kuona mtu ana funza au walikushambuli bas ni muda sahihi wa kuandika wosia watu wagawane Mali zako
Bado wapo sana tu, haina haja ya wosia. Kisiwa cha Mafia hadi leo funza wapo. Hasa msimu wa maua ya korosho na embe
 
Nadhani waliishia Kigoma. Haswa Kasulu na Kibondo, ni hatari. Zamani jamaa wengi wa hiyo miji walikuwa wanatembea kama Charlie Chaplin.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…