Funza ni Wadudu wenye asili ya America ya Kusini na ya Kati. Walikuja Africa kwa kupitia meli za Wareno na waathirika wa kwanza walikuwa Angola.Braza Kede mara ya mwisho lini kufika Kigoma? Maeneo ya Manyovu, uvinza, Kakonko Nyakanazi n.k
Huko bado funza wametia kambi
Sema kweli?? 🤣🤣🤣🤣kwa mbele yuko sawa ila nyuma ana kishundu cha haja
wakuu mnagombea starlet kweli au ndio mbio za kuku na mtetea wake? maana saivi unaenda wapi na starlet na mvua zote hizi?Starlet wakati hata tunda sijala walaku sana nyie na pacha wako maba mfyuuuu [emoji33]
Haahaa haya banaMama amefny kaz kubwa ya kutokomeza funza
🤣🤣🤣🤣🙌🙌Anko maba kanoga sio maskharaa
Amerithi umamani
Hawa hapa:Kwa faida ya wote hasa vijana wa kileo ni hivi hapo zamani sehemu kubwa za miji mingi haikuwa na lami.
Barabara nyingi zilikuwa ni za vumbi. Sasa hawa funza walikuwa ni wadudu wadogo mithiri ya viroboto wanaokaa kuzunguka sehemu ya jicho la kuku hawa wakijificha ndani ya hilo vumbi la barabarani. Wewe ukipita tu hapo basi tayari unao!
Funza aliingia kidoleni pale sehemu ya chini au juu ya ukucha na kuweka himaya yake hapo. Usipomtoa anataga mayai yasiyo idadi na kuzaliana hapo.
Ukichelewa zaidi kumtoa yale mazalia yanaenea maeneo mengine ya mguu. Usipokaa sawa mguu unapinda kuelekea upande mmoja yani kama ni wa kulia utapinda kuelekea kulia na kama ni wa kushoto utaelekea kushoto. bdae unaweza ukashindwa kabisa kutembea.
Hawa funza walikuingia kama umepita sehemu yenye vumbi hasa vumbi lile laini sana bila kuvaa viatu vya kufunika. Yaani ukivaa ndala, sendo, kobazi lazma uondoke nao. Leo hii ukimuona mhenga aliyepinda miguu kuna uwezekano mkubwa alipitiwa na funza miaka hiyoo!
Leo hii kwa maeneo mengi funza wamebaki kuwa ni hadithi ya kale kwani walitokomea wenyewe tu. Hadi sasa hakujawa na maelezo rasmi ya nini kilichosababisha funza kutokomea.
ndio inawezekana siwezi kukubishia kwa hilo. ila nachojua kwa maeneo mengi ya nchi wadudu hawa hawapo tena.Braza Kede mara ya mwisho lini kufika Kigoma? Maeneo ya Manyovu, uvinza, Kakonko Nyakanazi n.k
Huko bado funza wametia kambi
[emoji1]walishanijeruhi sana tu mkuu&asante kwa ushauri muruwaKama ushawahi kuona mtu ana funza au walikushambuli bas ni muda sahihi wa kuandika wosia watu wagawane Mali zako
ni kweli ila cha ajabu watu waliishi miaka mingi sana.Watu wa zamani mlipitia changamoto sana[emoji28]
Hayo yote kwakuwa dunia imefika mwishoni kweli ila cha ajabu watu waliishi miaka mingi sana.
magonjwa yalikuwa machache sio km leo hii.
vifo vilikuwa nadra sana kutokea sio kama leo hii.
mungu mkubwa.
Haahaa ni kweli wakiingia kuna kamuwasho fulani katamu ila ukizubaa tu kusikilizia ladha ya huo utamu unakuta ameshataga mayai na ana watoto tayari [emoji1]Funza n noma Sana kipindi hicho Ludewa uko funza wa kutosha,wakizidi kweli mguu unapinda, asubuhi huwa Wana washa miguu
yeah inawezekana kiongoziBado Kuna watu wana funza huko vijijini ndanindani
hatari sanaBwana jiga
labda kuna sababu zingine kiongozi ila ivyo vyote havikuwa shida vilikuwepoMatumizi ya maji na sabuni yamechangia sana kupungua kwa funza ingawa bado wapo sehemu zilizosahauliwa, zisizo na lami. Funza chawa na kunguni ni kielelezo cha uchafu wa mwili na kutokujali kanuni za afya.
kuwa uyaone mkuu. karibu.Daah ila stori zingine bwana[emoji1787][emoji1787] kwamba funza inafanya miguu ipinde?
-kiongozi shida hazijawahi kuisha.Mliteseka sana poleni aisee!!