Nitawezaje kunufaika endapo notatengeneza App ya TV?

black-tz

Member
Jul 20, 2021
54
69
Nataka nitengeneze App ya TV ambayo ndani yake kutakuwa na channels za kutizama mpira na vipindi mbalimbali vya TV (movies, news)

Je, zina faida? Au nitawezaje kunufaika nayo?
 
Utatoa wapi hizo "channel"? Una haki za kurusha huo mpira na hizo movie?
 
Hata ww mwenyewe heelewi utafanya biashara, pengine hiyo ni illegal business?
 
Mimi kama mzoefu ambaye nilifanya hiyo kitu miaka kadhaa nyuma, na kupata zaidi ya 100,000 downloads na watumiaji 20,000 hadi 40,000 kwa siku nakushauri yafuatayo.

1. Unaweza kutengeneza hiyo app, lakini hiyo ni illegal business kwa kuwa huna haki za matangazo za hizo channel, hivyo itashindikana kuiweka app yako kwenye play/app store

2. Unaweza kupata watumiaji kwa ku_share app yako kwa social networks lakini source ya uhakika ya kupata hizo channels ni ngumu kwa kuwa links nyingi now days ziko protected, hazitaweza play nje ya domain yao/app yao

3. Unaweza kuwa unachukua matangazo live kutoka kwenye decoder lakini kuwekwa nguvuni na mamlaka au decoder yako kufungiwa ni nje nje, (mfano huwa unaona kwenye channel za sports mara nyingi kuna wakati kuna namba flani huwa zina_display kwenye screen yako huwa zinakuwa tofauti kwa kila mtumiaji na zinatumika kutambua matangazo hayo yanarushwa kutoka kwenye decoder ya nani).

4. Hivyo kwa uzoefu wangu sio biashara sahihi sana kufanya kama utataka kuwa na sustainability.
 
Nimepata faida ya zile namba zinazojitokeza kwenye screen,,nilikuwa najiuliza sana niaje
 
Tafuta matatizo ya nayowakumba watu wa first world country Hawa washkaji kuspend $10-20$ kwenye app zinazo solve ishu zao NI simple
 
Back
Top Bottom