Wakuu hivi huwa mnadili vipi na watu wa aina hii? Please naomba mawazo yenu

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,076
17,246
Wadau bila kupoteza muda naomba tujadiliane kuhusu hili,
Kuna mtu mmoja mwenye matatizo ya akili(kichaa) alikuwa anakuja kwenye restaurant yangu sasa kutokana huruma za kibinadam nikawa namwambia muhudumu ampe tu chakula,
basi kidri siku zinavyozidi kwenda akawa anakuja kilasiku, na ikitokea labda mimi sipo au labda nikimkaushia(asipopewa msosi) huwa anaanza kuwasumbua wateja kwa kuwaomba hela au anakaa kwenye viti muda mrefu sana, kiasi mpaka anaziba siti za wateja wengine,
Hilo sio tatizo, sasa tatizo linakuja skuizi kuna mwingine nae anakuja so wanakuwa wawili, na anafanya action kama anazofanya kichaa mwenzake,
Wakuu sio kwamba sipendi kuwasaidia ila naona sasa watanivurugia mauzo pamoja na kunifukuzia wateja,
hasahasa ukizingatia appearance zao.
Naombeni mnishauri nifanye nini?
Nahisi nikiwafukuza wateja watanichukulia sina utu.

Sometimes unakuta nimekaa na marafiki zangu tunakula alafu ghafla unaona yule kichaa huyoo anaingia anakaa kwenye kiti, basi unakuta roho inaniuma kumfukuza nataka lakini nahisi itajenga bad image kwa marafiki hivyo nabaki kumtazama tu.
Hebu nishaurini wadau manake nisipokuwa makini Resta yangu itafilisika.
 
Weee hao wanakuchezea mchezo si ajabu ata si v ichaa...Huruma huruma mwingine huzaa dhambii
Mkuu huyu kichaa wa mwanzo nilikuwa namuona kitambo tangu ndo naanza kuijenga restaurant,
Ila huyu mwingine ni mpya machoni mwangu
 
Kwanini wanaongezeka. ? Hapo ninapata shaka huenda kuna mpango lakini wavumilie uone mwisho wao.
 
Endelea tu kuwaita vichaa wakati wenzio washakusoma na wanaendelea kupiga msosi wa bure. Muda si mrefu utakuwa unalisha familia nzima ya 'vichaa'.
Sasa mkuu kwamfano ungekuwa ndio wewe ungewachukulia hatua gani? Manake sometimes nafikiria hata nimuajiri mlinzi kwaajili ya kazi hiyo tu
 
Kwanini wanaongezeka. ? Hapo ninapata shaka huenda kuna mpango lakini wavumilie uone mwisho wao.
Mkuu nikiwavumilia sitouona mwisho wao, bali wao ndio watauona mwisho wangu baada ya kunifilisi
 
Tafta mtu Mvuta bangi mpe mchongo mzma akiona wanakuja awatimue we kaa mbali sehem ambayo watu hawakuoni wenzio ndo wanavyofanyaga hivyo
Zoezi hilo litanifanya niwe nakaa pale muda wote ili kuangalia usalama manake muda mwingi wanakuwa wafanyakazi, Sasa nahofia wanaeza wakagombana na huyo mvuta bangi then wakavunja vitu vya vioo,
Ila nitajitahidi niufanyie kazi huu ushauri
 
Back
Top Bottom