Wakurugenzi kataeni kuwa "chuma ulete".

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,401
wabunge watatu wameburutwa kwa pilato kisa ni kuomba cha juu kutoka kwa mkurugenzi ili wa mpambe nakufunika madudu. Jamaa kapiga hesabu kaona sasa anataka kuwa "chuma ulete" mmoja kadai 30m na walikuwa sijui wangapi na bado Majaliwa hajamzungukia na wanakijiji kumbebea mabango bahati mbaya Majaliwa anayasoma yale mabango na kuyafanyia kazi. Jamaa kaona isiwe tabu kalisanua.

Wasomi wengi wamejikuta wanafanya mambo ya hovyo nje ya utashi wao kisa misukumo ya kisiasa, anakuja diwani shule hakwenda kadanganya wapiga kura nao wakamsikiliza wakampa udiwani ndio atashinikiza mambo ya hovyo ilimradi asitoke kapa nawewe na shule yako unatetemeka unapelekwa tu kama mbuzi wa kafara, KATAENI NENDENI TAKUKURU.

Fikiria 300m zitumike kujenga uzio hata akili kidogo hutumii kuona kuwa hilo ni dudu? unatumia 450m fedha za kujenga nyumba za watumishi wa umma kulipa posho madiwani na kuwajengea ukumbi wa kugongea meza nawewe nyumba huna unakaa guest house halafu ukitumbuliwa ulalamike?

Tatizo la ulaji munakula kumi mutakaopelekwa mahakamani ni watatu na hao saba ukiwambia jamani nichangieni niweke mambo sawa wataruka mita mia. Kataeni kufanya mambo ya hovyo muwe na amani na mfanye kazi zenu kwa uhuru.
 
Back
Top Bottom