Wakina Tundu Lissu na TLS yao waonywa Kuhusu Mgomo, wajiandae kujibu Mashitaka

"mtu yeyote mwenye taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, anatakiwa kuzitoa polisi badala ya kuzungumza na vyombo vya habari."

LISSU NI ACCACIA NA ACCACIA WANASIMAMIWA IMMMA ADVOCATES na hao hao advocates ndio wanaomsaidia lissu kwenye kesi zake... za kuambiwa changanya na zako?

ACHENI KULETA UCHAMA KWENYE issue za msingi lissu hapo hajasimama kama mbunge amesimama kama rais wa wanasheria na ana mihemuko hivi kuwaambiwa wanasheria/mawakili wasiende kazini ni sawa kweli??

watu munatetea accacia mtasema mlizaliwa nao...wamewafanyia mangapi mpaka mko tayari kuiuza hii nchi na kuleta mafarikano kisa uchama....tujiangalie sana watanzania tunachezea amani, tuache kukurupuka.

Je watanzania wenzetu wanaofanya kazi katika kampuni ya ACACIA je nao hatujazaliwa nao? Hebu tujenge hoja asee watu Wako kwenye kazi zao na wanafanya kazi halali kikatiba
 
kiukweli lissu alifanya maamuzi mapema sana .. any way sijui labda walipewa taarifa hasi
 
Namheshimu sana Tundu Lissu ila nadhani kuna nyakati zingine huwa ' anakengeuka / anakosea ' sana hali ambayo inaweza pia kushusha hata ' Credibility ' yake katika Jamii. Hivi unajua kabisa kuwa tatizo lililotokea bado linafanyiwa uchunguzi na Police pamoja na Vyombo vingine kwanini uharakishe ' Kushutumu ' na kutangaza mgomo? Kwahiyo leo hii Wakili na Mwanasheria ' Nguli ' kama Yeye hajui taratibu za Kipolisi hasa yanapotokea ' majanga ' kama haya? Yeye huyo huyo anasema ana imani na Jeshi la Polisi lakini tena Yeye huyo huyo anashindwa kuliheshimu Jeshi hasa katika Kipindi hiki muhimu ambapo ' uchunguzi ' unaendelea.

Tundu Lissu unatuangusha kama siyo unatushangaza Watu tuliokuamini na jifunze kuwa ' mvumilivu ' hasa katika mambo yanayohitaji ' umakini ' mkubwa katika kuyakabili na acha kutumia uwezo wako mkubwa wa ' Kisheria ' na ' Ushawishi ' kuwahadaa Watanzania ambao bahati mbaya sana wengi wao nao uwezo wa ' Kuchanganua ' mambo ni mdogo na wanaishia tu kupelekwa pelekwa kama Ng'omba za mnadani.

Kwa mtazamo wangu tamko hili la Tundu Lissu lingekuwa na ' mantiki / logic ' kama angelitoa baada ya Polisi kutoa taarifa yao rasmi ya tukio zima na Yeye ( Tundu Lissu ) kuwahi hivi ' Kuzoza / Kupovuka / Kulaumu ' anakuwa hafanyi vyema hasa ' Kitaaluma ' Hivi kama Tundu Lissu anataka kuwaaminisha Watu kwamba huenda jambo hilo limepangwa / limeratibiwa na hao ' anaowajua ' Yeye ( namaanisha Mamlaka ) hivi na Sisi wengine tukisema kwamba huenda hilo ' tukio ' limeratibiwa na ' wahusika ' wenyewe pengine ili kuamsha hisia fulani ' ovu ' dhidi ya ' Mamlaka ' husika ambao wao wana matatizo / msuguano nayo au labda ili iwasaidie kusukuma ' agenda ' zao itakuwaje?

Mtani wangu wa ' Kinyiramba ' Tundu Lissu ' sometimes ' acha ' Kukurupuka ' tafadhali na jifunze kuheshimu Mamlaka.

Ni ukweli flan katika histor yake ya maisha kuwa lisu alishapatwa na matatzo flani ya kiakili na kutibiwa.

Hivyo ni ngumu sana mtu aina hiyo kurudia akili za 100% bila kuwa time fulan humsumbua hasa anaposhtushwa na jambo

Kunapotokea mambo ya mshutuko awe anawahiwa kuwekwa kwenye uangalizi maalum kabla ya kuropoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hata kama hilo tukio wamelifanya polisi, hivi hawana akili kabisa waende wamevalia sare zao!???!
Hii TLS ilikosea sana kuchagua MTU ambaye yupo kwenye active politics! Anabwatuka tu akidhani yupo jukwaani.

Sent from Moto G
wale walioingia na mitutu wakiongozwa na BASHITTE kuvamia kituo cha clouds walikuwa ni wamachinga dried???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatangaza amani huku wameshika mapanga

Hiki kichaka cha uchunguzi unaendelea halafu baada ya muda watu wamesahau mnakaa kimya kinasumbua sana nchi

Panapokuwa na dukuduku juu ya serikali kuhusika pawepo na chombo huru cha uchunguzi toka nje.
Maana hata kama kuna ushahidi serikali imehusika utaratibu huwa haufuatwi mfano lile la makonda kuvamia clause kwani alichukuliwa hatua ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofi si za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Juma alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake.

Profesa Juma alisema uhuru wa mahakama ni pamoja na kuheshimu mamlaka nyingine za nchi zinapokuwa zinafanya kazi zake. Alisema kwa kuwa tukio la kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa Immma ni tukio la kihalifu, hivyo wanasheria waiache Polisi na vyombo vingine vya upelelezi kufanya kazi yao.

“Kama kutatokea wateja watakaolalamika kuwa mawakili wao hawakufika mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano, hatua za kisheria dhidi ya mawakili hao zitachukuliwa ikiwemo kuwapeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili,” alieleza Kaimu Jaji Mkuu.

Kauli ya Jeshi la Polisi Kwa upande wao, Jeshi la Polisi limesema liachwe liendelee na kazi ya uchunguzi, badala ya kulihusisha na tukio hilo. Msemaji wa Jeshi hilo Makao Makuu, Kamishina Msaidizi Barnabas Mwakalukwa alisema Jeshi la Polisi ndicho chombo chenye mamlaka ya kufanya uchunguzi na hivyo kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, anatakiwa kuzitoa polisi badala ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Kauli hizo za Polisi na ya Kaimu Jaji Mkuu, zimekuja baada ya Rais wa TLS, Tundu Lissu kuwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Baraza lao la Uongozi lina taarifa kuwa kikundi cha watu wenye silaha za moto, wakiwa wamevalia sare za Jeshi la Polisi, kiliwateka nyara walinzi binafsi wa Kampuni ya IMMMA na kuingia ndani ya eneo la ofisi hizo.

Lissu alidai watu hao baada ya kuingia ndani, walitega milipuko na madumu manne ya mafuta ya petroli katika maeneo kadhaa ya jengo la ofisi hizo. Alidai muda mfupi baadaye, milipuko hiyo ililipuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa jengo la ofisi za IMMMA Advocates zilizoko Upanga pamoja na majengo jirani.

“Kama Lissu ana hizo taarifa alitakiwa azilete polisi kwa kuwa ndicho chombo cha uchunguzi badala ya kuzungumza na vyombo vya habari. Kazi ya polisi ni kufanya uchunguzi wa kina na ndiyo maana Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu alisema atatoa taarifa uchunguzi ukikamilika, hivyo watu wanapaswa kusubiri taarifa kamili, nje ya hapo tunakuwa tunafanya kazi nje ya utawala wa sheria,” alieleza Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mwakalukwa.

Mwakalukwa alivitaka vyombo vya habari, kuwatafuta walinzi hao ambao Lissu alidai walitekwa na watu wanaodhaniwa kuwa polisi ili waeleze tukio lilivyokuwa na ikibidi walinzi hao kutoa taarifa za kutekwa kwao polisi.

Alisema jambo hilo siyo dogo, hivyo watu waviache vyombo vya uchunguzi, viendelee na kazi yake kwani uchunguzi pekee ndiyo utakaobaini chanzo na wahusika. Ili kuonesha mshikamano, Baraza la Uongozi la TLS limewataka mawakili wote ambao ni wanachama wao nchini, wasuse kuhudhuria mahakamani na kwenye mabaraza ya aina zote kwa siku mbili, kesho na keshokutwa.

Lissu alidai kuwa lengo la kususa huko ni kupeleka ujumbe kwa jamii kuwa tukio lililotokea kwenye ofisi za IMMMA siyo dogo na hivyo wananchi ambao ni wateja wao hawana budi kwa siku hizo mbili kuungana nao kupinga jambo hilo. Alisema watamwandikia Kaimu Jaji Mkuu barua ya kumfahamisha kusudio lao la kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza yote kwa siku hizo mbili.

“Tunatambua kuwa wateja wetu wataathirika, na hiyo ndiyo maana ya kufikisha ujumbe wetu kwa jamii. Tunafahamu kuwa wajibu wa kwanza wa wakili ni kumwakilisha mteja wake mahakamani, lakini kama mawakili hawako salama, uwezo wa kuwawakilisha wateja wao mahakamani unakuwa haupo,” alieleza Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema.

Aidha, alililaani tukio hilo na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama, kuchunguza kwa kina ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao. Alisema mawakili wa IMMMA wanapaswa kupatiwa ulinzi dhidi ya vitisho au vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wao au kuwazuia kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma.

Kwa mujibu wa Lissu, Baraza la Uongozi la TLS litakutana na uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Kaimu Jaji Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuzungumzia vitendo vya kushambuliwa mawikili wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kisheria.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Shaaban alisema wanaungana na TLS kulaani shambulio hilo kwenye ofisi za IMMMA. Alisema IMMMA wana tawi lao Zanzibar na ndiyo maana aliamua kuungana na TLS kulaani tukio hilo.

Usiku wa kuamkia juzi kulitokea milipuko kwenye ofisi za IMMMA Advocates zilizopo Upanga katika Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam na kusababisha uharibifu. Imeelezwa kuwa vyombo vya uchunguzi vinaendelea na uchunguzi kubaini chanzo na wahusika wa tukio hilo.

Chanzo: Habari leo

Kaimu anatenda kama KAIMU anatafuta kuwa full JAJI tunamsamehe.Angekuwa ana akili zake peke yake angelaani kitendo cha IMMA advocate kulipuliwa na watu wenye SILAHA.Poor Kaimu Jaji
 
Namheshimu sana Tundu Lissu ila nadhani kuna nyakati zingine huwa ' anakengeuka / anakosea ' sana hali ambayo inaweza pia kushusha hata ' Credibility ' yake katika Jamii. Hivi unajua kabisa kuwa tatizo lililotokea bado linafanyiwa uchunguzi na Police pamoja na Vyombo vingine kwanini uharakishe ' Kushutumu ' na kutangaza mgomo? Kwahiyo leo hii Wakili na Mwanasheria ' Nguli ' kama Yeye hajui taratibu za Kipolisi hasa yanapotokea ' majanga ' kama haya? Yeye huyo huyo anasema ana imani na Jeshi la Polisi lakini tena Yeye huyo huyo anashindwa kuliheshimu Jeshi hasa katika Kipindi hiki muhimu ambapo ' uchunguzi ' unaendelea.

Tundu Lissu unatuangusha kama siyo unatushangaza Watu tuliokuamini na jifunze kuwa ' mvumilivu ' hasa katika mambo yanayohitaji ' umakini ' mkubwa katika kuyakabili na acha kutumia uwezo wako mkubwa wa ' Kisheria ' na ' Ushawishi ' kuwahadaa Watanzania ambao bahati mbaya sana wengi wao nao uwezo wa ' Kuchanganua ' mambo ni mdogo na wanaishia tu kupelekwa pelekwa kama Ng'omba za mnadani.

Kwa mtazamo wangu tamko hili la Tundu Lissu lingekuwa na ' mantiki / logic ' kama angelitoa baada ya Polisi kutoa taarifa yao rasmi ya tukio zima na Yeye ( Tundu Lissu ) kuwahi hivi ' Kuzoza / Kupovuka / Kulaumu ' anakuwa hafanyi vyema hasa ' Kitaaluma ' Hivi kama Tundu Lissu anataka kuwaaminisha Watu kwamba huenda jambo hilo limepangwa / limeratibiwa na hao ' anaowajua ' Yeye ( namaanisha Mamlaka ) hivi na Sisi wengine tukisema kwamba huenda hilo ' tukio ' limeratibiwa na ' wahusika ' wenyewe pengine ili kuamsha hisia fulani ' ovu ' dhidi ya ' Mamlaka ' husika ambao wao wana matatizo / msuguano nayo au labda ili iwasaidie kusukuma ' agenda ' zao itakuwaje?

Mtani wangu wa ' Kinyiramba ' Tundu Lissu ' sometimes ' acha ' Kukurupuka ' tafadhali na jifunze kuheshimu Mamlaka.
kama mamlaka haikuheshimu unaazaje kuiheshimu?
 
Wanatangaza amani huku wameshika mapanga

Hiki kichaka cha uchunguzi unaendelea halafu baada ya muda watu wamesahau mnakaa kimya kinasumbua sana nchi

Panapokuwa na dukuduku juu ya serikali kuhusika pawepo na chombo huru cha uchunguzi toka nje.
Maana hata kama kuna ushahidi serikali imehusika utaratibu huwa haufuatwi mfano lile la makonda kuvamia clause kwani alichukuliwa hatua ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
walipatanishwa na sizonje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaji anaingiza siasa mahakamani, Lissu anaingiza siasa TLS...
Somo: "Hakuna Mwanasiasa Msomi"
Ushauri: Wachague moja kati ya siasa au taaluma
 
Hatuna imani na serikali...uchunguzi kutekwa kwa wakina Roma mkatoliki kimya..Ben wa saanane???
 
Polisi wahusishwe halafu wajichunguze wao wapi na wapi kinatakiwa chombo huru kuchunguza tukio hilo.

Kazi ya uchunguzi wamepewa polisi, hiyo ndio kazi yao, wewe unataka apewa nani? Acheni maneno yenu yasio kuwa na tija katika nchi yetu.
 
Hatuna imani na serikali...uchunguzi kutekwa kwa wakina Roma mkatoliki kimya..Ben wa saanane???
Futa maneno yako kabisa, mbona mahakama ilipotoa hukumu ya ushindi Bulaya hamkukataa kwa kusema kwamba hamuamini serikali? huo ndo ufnyu wa fikra zenu ulipoishia.
 
Back
Top Bottom