Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Nakusalimu Wakili Msomi mwenzangu na Rais wangu wa Mawakili Tanganyika na Mbunge wa nchini mwangu, Tundu Lissu. Nimesoma kwa hatua, undani, umakini na kwa uelewa mkubwa hoja yako uliyoiweka hapa kuhusu masuala ya madini na kile ambacho Rais Magufuli anakisimamia kwa sasa. Uzi wako ni huu: Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima...
Wakili Msomi Lissu (nimechagua kukuita Wakili Msomi kwakuwa ndicho kitu 'tunachoshare' mimi nawe), katika uzi wako niliousoma humu JF, umeuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Umeuliza kisomi katika namna ya kutafuta majibu kutoka upande wa pili-upande wa Serikali na wa chama tawala. Nimeyasoma maswali yako yote na nakiri kuwa maswali mengi ni magumu kujibika kwa wakati huu tulionao.
Nimeielewa mantiki ya uzi wako: ni kutaka usilaumiwe kwa makosa yaliyofanywa na wengine ambao sasa ndio hasa wanaotaka kuyarekebisha. Umelenga kusisitiza kuwa msimamo wako juu ya rasilimali za Taifa ni ule ule wa kuzilinda na kupinga kila sheria, sera au mkataba mbovu unaohusu mambo hayo. Ukakumbusha pia jinsi harakati zako za kutetea rasilimali za Taifa 'ulivyokuponza' kwa kushtakiwa kwa uchochezi. Ujumbe wako uko peupe na ni rahisi kuonekana.
Wakili Msomi Lissu, ni jambo jepesi, la wazi na la moja kwa moja kukubaliana kuwa kuna makosa makubwa yalifanywa na tawala zilizotangulia katika kuzisimamia rasilimali za nchi hii kama madini, gesi asilia na mafuta. Ushahidi wa hilo ni Sheria zinazosimamia rasilimali hizo ambazo ndizo chanzo za haya yote. Ni chanzo cha mikataba mibovu na isiyo ya haki ya madini, gesi asilia na mafuta. Ndizo Sheria ulizozisema na kuziita Unholy Trinity.
Wakili Msomi Lissu, Rais Magufuli na Serikali yake, kwa kuzingatia ubovu wa Sheria hizo, ameamua kwa dhati ya moyo wake kufanya marekebisho. Marekebisho yanayolenga kulinda rasilimali zetu. Pamoja na kwamba yeye pamoja na wengineo wa sasa walishiriki kuzipitisha Sheria hizo, kujirekebisha ni jambo jema,la kiungwana, la kizalendo na la kuliunga mkono. Rais anapoamua kufanya kazi ya kulinda rasilimali zetu, kila mmoja wetu anapaswa kumuunga mkono. Na kutomuunga kunaruhusiwa.
Wakili Msomi Lissu, Rais, hata kama anatokea kwa wapinzani wenu CCM, ni kiongozi wetu sote watanzania kwa ujumla wetu kwa miaka yake mitano: 2015-2020. Anachokifanya, kama hiki cha madini, ni kwa ajili yetu sote. Huu si wakati wa kuzodoana na kusimangana kama si kusemana; ni wakati wetu wa kusimama imara pamoja na kushikamana kwelikweli. Ni wakati wa kuwaonyesha wa nje yetu kuwa watanzania wanaweza wakiamua, hata kwa kujirekebisha!
Kinachotakiwa sasa, Wakili Msomi Lissu, ni kusubiri muda wa kutimiza wajibu wako katika masuala haya. Kwakuwa wewe ni Msomi wa Sheria na Mbunge mwerevu,mjenzi mzuri wa hoja, mtafiti uliyebobea na msomaji wa neon kwa neno, isubiri Miswada iletwe Bungeni na uitendee haki. Kuanzia kwenye Kamati za Bunge hadi kwenye majadiliano Bungeni, tunatarajia wewe na Wabunge wenzako, mtaijadili kwa kina Miswada hiyo ya kurekebisha Sheria zetu na kuiweka katika 'sura' za kizalendo na za kulinda rasilimali zetu. Huu ndio wakati wa kuwa pamoja!
Rais Magufuli anasema na kutenda kama anavyosema. Kwa hili la madini, atatimiza ahadi yake ya jana kuhusu Sheria za Madini, Gesi Asilia na Mafuta. Na waliohusika kutufikisha hapa tulipo, kwa uongozi wa Rais Magufuli, hawatabaki salama. Labda kwa wale wenye kinga kikatiba. Kuwashughulikia ni kama mambo yetu ya 'kifamilia'!