Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Nikiri kuona humuhumu JF, nakala ambazo hazijakamilika za nyaraka za kufungulia shauri Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma za Wakili Msomi Wasonga dhidi ya Tanganyika Law Society(TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nyaraka hizo hazijakamilika kwakuwa hazijasainiwa na yeye Wakili Msomi Wasonga wala Mahakama wala Wajibu Maombi.
Wakili Wasonga, kulingana na nyaraka hizo, analenga mambo makuu matatu: Mosi, Wakili Wasonga analenga kuiomba Makakama Kuu itoe amri ya kusitisha Uchaguzi wa TLS unaotarajiwa kufanyika tarehe 18/3/2017 kule mkoani Arusha. Pili, analenga kuiomba Mahakama Kuu iuongezee muda uongozi wa TLS wa sasa ili marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi yafanyike.
Jambo la tatu ni kuiomba Mahakama Kuu izibatilishe Kanuni za Uchaguzi za TLS za mwaka 2016 kwakuwa si Kanuni halali. Kulingana na nyaraka hizo, Wakili Msomi Wasonga anadai kuwa Kanuni hizo zimesainiwa na anayetajwa kama Rais wa TLS: Wakili Msomi Charles Rwechungura ambaye hakuwa na mamlaka ya kusaini Kanuni hizo kwakuwa wakati Kanuni zinatolewa hakuwa Rais na hakukuwa na ruhusa ya Rais wa sasa, Wakili Msomi John Seka kumruhusu kuzisaini.
Hivyobasi, Wakili Msomi Wasonga analenga kusimamisha uchaguzi wa TLS kwakuwa unataka kufanyika chini ya Kanuni batili na hivyo kupatikana kwa viongozi wa TLS batili. Nikiwa kama Wakili Msomi (Roll Number 3874), nafahamu fika kuwa hapa si mahali sahihi pa kujibu mambo ya Wakili Msomi Wasonga. Kama kesi itafunguliwa rasmi Mahakamani, mambo yatajadiliwa huko na kutolewa uamuzi.
Ninachojaribu kudadisi ni timing ya shauri hilo. Ilishasemwa kuwa kuna kila mpango wa kukwamisha uchaguzi wa TLS kwakuwa tu Tundu Lissu anagombea Urais wa chama hicho cha Mawakili Tanganyika. Mwanzoni zilikuwa kama propaganda changa. Lakini, sasa propaganda hizi zimekomaa.
Kanuni anazozipinga Wakili Msomi Wasonga zilichapwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 30/12/2016 kama Tangazo la Serikali Nambari 332 la mwaka 2016. Kuanzia hapo, kumepita miezi miwili. Wakili Msomi Wasonga alikuwa wapi kuzipinga (kama kweli zina mapungufu) hadi asubiri siku chache kabla ya uchaguzi? Kwanini iwe sasa?
Kutokana na timing yake, Wakili Msomi Wasonga hawezi kujiepusha na kuwa na ill-will kama Mawakili na wananchi wa kawaida wanavyojadili na kuamini. Nampa rai tukutane Arusha na tuchague viongozi wetu wa TLS kwa mujibu wa Sheria zetu, mashahi na matakwa yetu. Ameshachelewa kulisimamisha treni hili la TLS!
======================================================
https://www.jamiiforums.com/attachments/img-20170309-wa0000-jpg.478568/