Wakili William Maduhu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ameeleza kuwa Sheria ya Mtoto nchini Tanzania inakataza upigaji picha za watoto na kuzichapisha mitandaoni kwa sababu ya kulinda faragha za watoto hao.
Akizungumza leo Machi 19, 2026, kupitia kipindi cha Jambo Asubuhi kinachorushwa Jambo TV, Wakili Maduhu amesema amewatahadharisha wazazi kuwa kupiga picha watoto wao na kuzichapisha ni kinyume cha sheria.Aidha, ametoa wito kwa mamlaka husika kufuatilia matukio haya kwani yamekithiri nchini.