Swala la lugha mbilii tofauti huko chini na huku juu its total nonsense, na ndio namba 1 cause ya watu kufeli tanzania, tukifika huku juu tunaanza kurudia ya nyuma na hapo ndipo watoto walisoma shule za bei kubwa magep yanapoanza since wako safi katika ngeli, kama ni ngeli basi weka chini hadi juu, likewise kama ni kiswahili the same thing ila tukiweka kiswahili tukumbuke kua tusitegemee vitabu tu, information nyingi tutashindwa kuzipata mfano kwenye internet, research watu tunachimba sana huku looking for answers, angalia vitu kama english documentaries za science, kama hujui ngeli hata kdg hutodaka term za kisayansi zile, bongo hatuweki info zozote kwenye net zinazohusu elimu, hatufanyi discussion ya topics nyingi, mfano bongo ulisikia wapi mtu anafundisha astronimy kwa kiswahili au hata kwa ngeli afu akaupload? tukiweka ngeli itarahisisha since resources zote zipo kwa lugha yao, kiswahili tutatumia nje tu ya darasa maana watu wataanza ohh lugha ya taifa, ohh uzalendo, english nani alikwambia ni lugha ya mwingereza au mmarekani? si waweke patent sasa mtu asitumie bila ruhusa yao? lugha ni ya binadamu full stop.
Kwa kweli Kiswahili kilinitatiza sana katika shule ya upili; haswa yale maneno ya ngeli:crazy:. wanafunzi wa siku hizi wana bahati kwa kuwa hao hufundishwa ngeli kwa kufuatilia viwakilishi na sio nomino kama siku zetu. Nilikuwa kwa kawaida baadhi ya watu watano wa mwisho kwa tulipokuwa tukifanya mitihani.Sijabobea katika lugha ila you sound like umelelewa na kukulia bongo!!
vitabu vya kiswahili vya science kwa shule ya msingi vipo vingi tu mimi mwenyewe nimevitumia wakati nasoma shule ya msingi...hujataka tu kuvitafuta
Lugha ni tatizo sana, binafsi nilipokua shule ya msingi nilikuwa na uelewa mzuri kabisa, vitu nilivyosoma sijapata kuvisahahu mpaka leo. Shule ya msingi nimesoma mambo mengi sana ambayo sekondari wenda yanaenda kwa level ile ile, ila watu wanafeli tu kwa sababu ya lugha.
Mfano, shule ya msingi nimejibu maswali ya nini na wapi mwanamtapa? nimejibu dola ya mali, shona na zulu. Mfalme chaka, dola ya benin nk.
Wakati darasa la tano nimesoma nne jeografia ya Tanzania,jeografia ya Afrika darasa la tano, darasa la sita jeografia ya ulimwengu, na darasa la saba nimesoma afrika mashariki.
Sayansi nimesoma vitu vile vile wengi wakifika sekondari ama elimu ya pili uliyoiita vinawashinda. Mfano nimesoma mfumo wa umengenyaji, maumbile ya mtu wanyama mamaria, amfibia, leptilia nk.
Ama nimesoma Mchapuko = mwendokasi gawia mda yani acceleration = velocity over time. Nimesoma Uzito na tungamo yani weight and mass. Nimesoma, msongamano =tungamo gawia ujazo yani density = mass over volume.
Pia nimesoma mkondo wa umeme na tofauti za kipoteshali yani current and potential difference. Bila kusahau ile kitu ya muungano wa chembechembe ndogo sana .... yani atom.
Kwa kweli elimu ya msingi ilikuwa tamu sana na nilikuwa sihitaji kujisomea, kwa sababu mwalimu alikuwa akiongea nilikuwa na muelewa kwa ufasaha na hivyo sikuhitaji kujisomea badala yake nilipotoka skuli nilienda kupiga sembo yani mpira wa kujitengeneza wa karatasi na matambala.
Cha moto kwa kweli nilikiona ktk elimu ya sekondari, kwa sababu mwalimu alikuwa akiongea nilikuwa sielewi anaongea kwa undani nini anaongelea. Na material ya sekondari ni yaleyale tu ya shule ya msingi japo yame advance kidogo, kitu ambacho kilitakiwa kisiwe tatizo kabisa. Lakini cha maajabu kiligeuka kuwa tatizo kubwa ikabidi kuwa nalala darasani na maji kwenye karai na mbu kunikung'uta.
Mfano somo la jeografia kwa sekondari utakuta wamepiga picha wananchi wakivuna kakao ama karafuu harafu wanakuuliza unafikiri hilo ni zao gani na wanafany nini? ni swali lile lile ktk shule za msingi tulikokuwa tukiulizwa. Ama mfano sendondari watakuliza collapse of mwanamutapa empire--- kitu kile kile tulikuwa tunaulizwa darasa la tano sababu za kuanguka dola ya mwanamtapa. Kumbe tatizo linakuja kuwa na lugha.
Serikali za afrika nafikiri zinabidi zichague lugha ya kufundishia masomo yote kwa ngazi zote, na hiyo lugha lazima wahikikishe inaeleweka vyema toka chekechea ili kuweza kuwa na mabadiriko chanya ktk nyanja ya elimu. Studying by heart, hakutatunusuru kamwe.
Kwa Tz shida iliyopo ni shule ya msingi kutumika kiswahili na sekondari kutumika kiingereza. Kenya endeleeni hivyo hivyo, mkitaka fundisheni kwa kiswahili kuanzia awali mpaka chuo kikuu msije mkatuiga sisi mtapotea bure.
Fundisheni Kiswahili kama somo mpaka Chuo kikuu.
Acha watu waendelee kujifunza kwa kiingereza.
Wakati ukifika lugha imekua watajua cha kufanya.
Asante sana kwa maoni yako. Kwa kweli, sielewi ni kwanini wakuu serikalini hawawezi kuona comon-sense issues kama hizi. Tuko na kasumba mbaya sana sisi waafrika. Itakuwaje nchi kama Iceland, inatumia lugha ya Icelandic inayoongelewa na watu 300,000 kutumia lugha hiyo kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na ilhali sisi wenye lugha inayoongelwa na watu zaidi ya milioni mia moja kukidunisha?
Upuuzi wa kukariri hapa Kenya umezidi. Jambo la kukera zaidi ni kuona mtu anafikiri ya kuwa kujua kiingereza ndio kuelimika. Niliwezachakurachakura kwenye mtandao nikapata curriculum ya California ya sayansi ndiposa nikaelewa kwanini sisi ni nchi maskini. Yale mabo ambayo wanajifunza katika darasa la pili - kama photosynthesis, sisi tunaanzia darasa la tano au nne. Yale wanayosoma katika shule ya chekechea - kama vile evaporation, sisi hatuwezi tukasoma kwasababu mtoto mdogo hawezi kushika maana ya evaporate. Lakini, ukimuuliza vizuri, utapata kuwa yuajua maana yake, ila tu lugha ndio shida.
Ni lazima tujikomboe mawazo
Sijabobea katika lugha ila you sound like umelelewa na kukulia bongo!!