Kwa wakazi wa Arusha wengi wanalalmika kunywa maji yasiyo salama hasa kipindi cha mvua. pamoja na kulipa bili kubwa za maji na nyingine za kubambikiwa kwa njia ya sms bado idara ya maji imelala. Invyoonyesha pump zilizopo kwenye vyanzo vya maji zinapeleka maji machafu kwa wakazi. nawasihi idara ya maji mlichunguze hili na mlifanyie kazi bila hivyo magonjwa ya Typhoid hayataisha na pia hii ni tahadhari kwa ugonjwa wa kipindupindu msije kushangaa jiji Zima wote ni wagonjwa.