mimi ni mkristo na nimishaisoma yote na kuielewa kura yangu ni hapana.
Ibara ya 21waiondoe kwanza, mtu unapewa haki kwa mkono wa kulia baadae unapokonywa kwa mkono wa kushoto. huu ni ujinga sana.
Kwa mfano: wakulima wameambiwa kuwa, wana hakiya kupata ardhi kwa ajili ya kilimo chao ila sasa tatizo ni hili, usipopata hiyo ardhi huna haki ys kwenda kushtaki popote na mahakama zote zimezuiwa kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi yoyot juu ya sura hii ya pili.
hivyo hivyo, wafugaji, huduma za afya, elimu, maji nk.
hizi nazo wamesema kuwa wananchi wanayohaki kupata elimu bora, maji safi na salama, maeneo ya kulishia mifugo na huduma bora za afya, ila usipopewa hivi vitu hutashitaki popopte.
Ibara hii inaturudisha tulipo sasa kwani serikali inakimbia uwajibikaji kwa wananchi na kuruhusu hata pesa zilizotengwa kwa huduma hizi ziendelee kuliwa kama sasa na mchwa wa Halmashauri na idara zingine.
PIA: kamati ya uteuzi wa TUME YA UCHAGUZI wamo akina SPIKA NA NAIBU WAKE hii haikubaliki, TUME ya warioba iliweka vile kwa kuzingatia mfumo wa serikali tatu na kwamba Hawatatokana na vyama vya siasa, sasa kwa mfumo wao huu wa serikali mbili kuwaacha SPIKA NA NAIBU wake eti wawe wateuzi wa wajumbe wa TUME HURU ya uchaguzi haikubaliki.