VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Pia walipita mitaani wakichukuwa namba za wanachama wao, sasa namba zao zimehakikiwa tayari kwa kupiga kura, ukawa wamejiandikisha lakini kura hawatapiga, hawapo kwenye daftari.
Mzee VUTA-NKUVUTE, UKAWA bado hatujaanza mbona? Hizo ulizoona ni rasha rasha tu..
Kipenga kikipulizwa Majukwaa mtayaona machungu.. andaeni majibu ya ESCROW- Ilikuwaje watu wakabeba mabilioni kwenye rumbesa na viroba, Marehemu kupiga kura BMK, Najua Rasimu ya Warioba majibu hamna... lakini mtuambie pia Twiga wetu wanapandishwa ndege kwa nauli ya nani na kwa maslahi ya nani, Na nani anahusika na ukatili wa tembo wetu.. Mtuambie pia Bilioni 250 wizara inayoongozwa na mgombea wenu zimeyeyukia wapi( refer CAG report)
Lakini msisahau kutuambia Budget ya Safari ya Amiri jeshi mkuu ya mwaka mzima inaishaje ndani ya miezi miwili? Inabidi Mjiandae sana aisee... Manake majuzi mmepitisha Miswada ya Gas ana mafuta kwa hati za dharura, mtuambie ni kwa maslahi ya nani na kwa kipi.
Mjiandae vizuri aisee na mtuambie pia Kwa nini huduma za afya bado ni hoi kuliko jana pia msisahau kutuambia Dr Ulimboka Aliteswa kwa Lipi na kwa maslahi ya nani.
UKAWA msidhani hatuwaoni. Tunawaona ila tunawapa nafasi ya kutamba kwa namba. Kuonesha watu kuwa mna mafuriko popote apitapo mgombea wenu Lowassa. Huu ni wakati wenu kucheza scene yenu halafu nasi CCM tuanze scenes zetu. Kalikali. Za kiushindi. Tayari muda unakaribia. Muda wetu umepiga hodi na tunainuka kuufungulia. Muda umeshafika. Subirini muone.
Malizeni kuteua wagombea wenu wa Ubunge na Udiwani halafu tuwaoneshe mchezo. Tutawashawishi wagombea wenu ili wafanye 'mambo' na wetu wapite bila KUPINGWA. Mbele ya rupia,wapo watakaojaza hovyo fomu zao ili wawekewe mapingamizi na mwishoni kuondolewa. Wapo watakaochelewa makusudi kurudisha fomu na hivyo kujifuta kwenye kugombea. Wapo watakaotengeneza wenyewe filamu za kupotea.
Muda umefika huku ukiwa unahitajika. Wakati wa kupiga na kuhesabu kura pia hatuna wasiwasi. Tutafanya 'mambo' hata bila ya kuwatumia mgambo. Kitaeleweka tu mwaka huu. CCM itashinda kwa kishindo kikubwa kwakuwa ina nia na maarifa ya kufanya hivyo kama alivyodokeza Mwenyekti wetu alipohutubia hapa Lumumba siku Dr. Magufuli alipochukua fomu ya kugombea Urais. Tumejipanga.
CCM, mbele kwa mbele!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam