Uzoefu uliopatikana katika kutekeleza makubaliano ya UKAWA unayonyesha kwamba wakati umefika sasa wa kuyafanyia marekebisho makubaliano hayo ili yaweze kukidhi mahitaji halisi ya ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA.
Makubaliano ya UKAWA katika kuweka mgombea mmoja kwenye maeneo mbali mbali ya uchaguzi yamewekwa kwa vigezo mbali mbali vikiwemo :
1. Chama kuwa na mgombea anayekubalika zaidi
2. Idadi ya wanachama
3. Chama kilichoshinda uchaguzi uliopita
4. Maridhiano/muafaka au kura ya maoni
Kwa upande wa serikali za mitaa UKAWA wamefanya kazi nzuri kuhakikisha ushirikiano huu unakwenda vizuri. Hata hivyo kuna maeneo ambayo vyama vimeshindwa kukubaliana kuweka mgombea mmoja na hili ni jambo ambalo inabidi lishughulikiwe katika makubaliano kwa wakati huu kabla ya uchaguzi wa udiwani, ubunge na urais kwani kama limetokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, linaweza kutokea kwenye uchaguzi mkuu.
Kuna eneo kama la manzese kwa mfano ambapo CUF wanasema wao ndio walipata kura nyingi kwenye uchaguzi uliopita na wakati huo huo CDM wanaona wao ndio wanastahili kusimamisha mgombea nadhani labda wanafikiri kwamba wao wana wanachama wengi kwa sasa hivi katika eneo hilo na wanaona wao ndio wanakubalika zaidi. Kuna maeneo mengine nimesikia vile vile kwamba kuna kitu kama hiki kimetokea. Ukiangalia vile vile tamko la kiongozi wa CUF (Kambaya) kulalamikia wana UKAWA wenzake linaashiria tunaweza kuwa na matatizo kama haya hapo baadaye na hivyo lazima tutengeneze utaratibu wa kuyashughulikia.....
Mimi naamini ukiangalia vigezo vya chama kukubalika/kuenea/kuwa na wanachama wengi, na matokeo ya nyuma ni obvious kwamba CDM ndio watatakiwa wamsimamishe mgombea Urais na vile vile kusimamisha wagombea wengi wa ubunge na udiwani kwa upande wa Tanganyika. Kwa upande wa Zanzibar obviously CUF inabidi ipeperusha bendera ya UKAWA kwwenye maeneo yote ya Zanzibar. Huwezi kusimamisha mgombea wa CDM au NCCR au NLD kwa upande wa Zanzibar hata kama ni mzuri kiasi gani wakati political infastructure iliyopo yote ni ya CUF !. Na kwa upande wa Tanganyika ni hivyo hivyo, sioni kwamba kuna hata haja ya kujadili ni Chama gani kisimamishe mgombea yrais.....Obviously inabidi kiwe CDM. Nani asimamishwe ndani ya CDM ndio inabidi iwe swala la majadiliano na hapo sasa ndipo wana UKAWA wengine inabidi washiriki kuona nani ndani ya CDM atapeperusha bendera ya UKAWA kwa sababu mgombea huyo vile vile ndie atakayekuwa mgombea wa UKAWA....
Sasa unapoona kiongozi mkubwa kama Kambaya anatoa tamko kama la leo na kuliita ni la chama chake, then inawezekana kabisa viongozi wengine wa CUF waliliona na walilikubali kabla Kambaya hajalitoa na kwa maoni yangu, hili ni jambo serious ambalo linatakiwa lipatiwe ufumbuzi.....
Kwa uzoefu uliopatikana kwenye serikali za mitaa pamoja na haya mengine tunayoyaona sasa, kuna uwezekano mkubwa sana hapo baadaye vyama vikashindwa kukubaliana kwamba nani asimame katika ngazi ya udiwani, ubunge au hata urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Haya yanaweza kutokea kwa sababu za msingi (kama ilivyotokea manzese) au kwa sababu za ki-pumba-vu, pu-mbavu- tu au za ki-usaliti !
Kwa maoni yangu kiwekwe kifungu kwenye makubaliano ambacho kitasema kwamba pale ambapo vyama vitashindwa kabisa kukubaliana juu ya mgombea mmoja basi kila Chama kisimamishe mgombea na wakati wa campaign chama chochote kikiona kwamba chama kingine/mgombea mwingine ndio anakubalika basi kumuunge mkono. Na kama vyote vitaendelea kujiona vinakubalika mpaka mwisho basi viendelee tu mpaka mwisho......
Hili naona ni muhimu sana, kwani tusipoliweka officially kuna uwezekano mkubwa likatokea maeneo mengi tu UN-OFFICIALLY jambo ambalo ni baya zaidi. Hili jambo likiwekwa officially maeneo ambayo hatuna migogoro tutatendelea vizuri kushirikiana kwani haya maeneo ambayo tutashindwa kuelewana hayataleta madhara kwenye maeneo mengine.....
Tukubali kutokubaliana na tuhakikishe kutokukubaliana kwetu hakuathiri maeneo ambayo tunakubaliana. Na njia nzuri ninaamini ni kuweka namna rasmi (official) ya kukubaliana kutokukubaliana !