Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,266
hivi kipi,o cha uadilifu nini bwana mziwanda?
SITTA hana lolote bado anahofuu kubwa ya maisha yake bila kuwa CCM..Ni unafiki usiokuwa na KIPIMOOOOO...
SITTA hana lolote bado anahofuu kubwa ya maisha yake bila kuwa CCM..Ni unafiki usiokuwa na KIPIMOOOOO...
Wana Great Thinker,
Kwa maoni yangu na ushauri wangu kutokana na hii mada/topic, mimi naona tatizo lipo kwenye Katiba ya Nchi, naona Katiba inampa Nguvu na Madaraka makubwa Rais ambaye ndie Mwenyekiti wa Chama ambacho kinatawala.
Tunapaswa kuwa na Katiba ambayo inawapa wananchi nguvu ya kuwawajibisha Viongozi, hata Rais asipo/wasipo fanya kazi au kutimiza wajibu wao. Bado tuna kazi kubwa ya kubadilisha Katiba kutoka Mfumo wa chama kimoja kwenda Vyama vingi ingawa Katiba yetu tunaiwekea viraka hapa na pale.
Uoga wa viongozi wetu wa kutoa maoni, ushauri kwa kuhofia Usalama wao na familia zao na biashara zao na mali zao, na kufanya Siasa kama ni njia ya kutafuta ulaji, ili mradi mkono uende kinywaji.
thats y nikasema ni unafiki kuendelea kulamba miguu ya wakubwa kwa kuogopa changamoto
Kwa hiyo tusubiri kusambaratika sio?Magamba igawanyike mara ngapi bana!!!? we husikii Lowassa ana kundi lake, Membe ana kundi lake, Mkapa ana kundi lake, Sitta ana kundi lake. Magamba imeshagawanyika miaka mingi iliyopita.
Redsiyo unafiki, wale wazuri wachache waliopo CCM wanafikiri muda bado wana matumaini ya kuibadilisha CCM ambayo bado ni chama makini kiitikadi na kinadharia. Haya matumaini bado ni makubwa kiasi fulani, lakini yakianza kufifia kabisa katika miaka miwili ijayo maamuzi mazito yatachukuliwa...kinachoiunganisha CCM sasa hivi ni matumaini kama haya waliyonayo makundi yote ndani ya CCM. Nyerere alisema wapinzani wa kweli watatoka CCM..tukae tusubiri