Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Kutokana na kushamiri uyoga wa vyama vya siasa nchini amabavyo havikidhi haja ya msingi ya kisheria au kupoteza sifa hizo kabisa na kugeuka kuwa vitimbakwiri wa vyama vikubwa, haja ya kuchukuliwa hatua stahili na Msajili mwenye dhamana ya kuhakikisha kuwa vigezo na masharti ya kuwa chama siasa yanazingatiwa.
Unapoanzisha chama unatakiwa kufuata sharti la msingi
" The party must obtain not less than two hundred registered members who are qualified to be registered as voters for purpose of Parliamentary elections from each of at least ten Regions of
the United Republic out of which at least two Regions are in Tanzania Zanzibar, being one Region each in Zanzibar and Pemba"
Vyama vingi vimeshindwa kuikamilisha sheria hii ya msingi na matokeo yake kulijitokeza udanganyifu, rushwa au kuonewa huruma na msajili wakati wa uhakiki na hivyo kusajiliwa kinyume na sheria na taratibu.
Wahenga wanasema "mficha ugonjwa utamuumbua" Matokeo ya chaguzi zote mbili imedhihirisha kuwa vyama vingi vimepoteza " deposit" na havikuweza kupata idadi ya kura hata kufikia kura 200, idadi ya msingi ya kukubalika kuwa chama cha siasa.
Katika uchaguzi halali wa marudio uliofanyika Zanzibar kulikuwa na kama vyama saba, CCM, UDP ADC, CCK, DP, TLP na SAU,kati ya hivyo kuna vyama havikufikisha hata kura 50 kwa mgombea urais, kwa wawakilishi na madiwani aibu hata kusimulia. Hali hii imejitokeza pia kwenye uchaguzi wa muungano. Hii inamaanisha kuwa vyama hivi hata kushindwa kupata kura angalau zile za watu waliokidhamini, walitumia rushwa, udanganyifu au upendeleo kupata usjili wa kudumu.
Sasa umefika wakati wa Msajili kuchukua hatua inayostahili,na upate kulinda hadhi ya jina lako na kuondosha dhana potofu ilionea kuwa wewe ni mwega wa chama fulani.