Ni lazima uwe na biashara inayoendelea, inayoendeshwa kihalali na uwe na leseni ya biashara
Uwe unafanya kazi katika eneo la biashara la kudumu lenye miundombinu inayofaa, uwezo wa kifedha na rasilimali watu ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi na usalama.
Mtu/Biashara lazima isiwe na rekodi mbaya ya madeni kwenye benki au taasisi yoyote ya kifedha kwa muda wote wa makubaliano ya uwakala
Mtu/Biashara haitakiwi kuendesha huduma ya Benki kama shughuli yake pekee na lazima uwe na kitambulisho cha NIDA
Mtaji wa chini kabisa ni Tsh Milioni 2 na ada ya maombi ya uwakala ni Tsh 350,000 ambayo haiwezi kurejeshwa mara wakala atakapoidhinishwa na kusaini makubaliano.