Wajumbe wa Kamati kuu CHADEMA, kufanya Ziara Kanda ya Pwani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Taarifa inatolewakwavyombo vya habari na umma kuwa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, Wajumbe wa Kamati Kuu wakiambatana na wabunge waliopangwa katika timu, wataanza ziara ya kikazi itakayohusisha vikao vya ndani katika majimbo ya Kanda ya Pwani, ikiwa ni sehemu ya uimarishaji wa chama na maandalizi ya uchaguzi wa kanda hiyo utakaofanyika Machi 19, mwaka huu.

Ziara hiyo yasiku nne itakayoanza kwenye majimbo Machi 16-17, itafuatiwana Kikao cha Kamati Kuu ya Chama itakayoketi Machi 18 kufanya uteuzi wawagombeawanafasi za Mwenyekiti wa Kanda, Makamu Mwenyekiti wa Kanda na Mweka Hazina wa Kanda, kisha Mkutano Mkuu Maalum wa Kanda ya Pwani (mikoa ya Pwani, Temeke, Ilala na Kinondoni) utakutana Machi 19, kuchagua viongozi katika nafasi zilizotajwa.

Mbali ya agenda ya ukaguzi wa chama na uchaguzi wa kanda, vikao hivyo pia vitajadili hali ya kisiasa katika maeneo husika na taifa kwa ujumla, ilivyo hivi sasa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe ataongoza timu itakayofika katika majimbo ya Kibaha Mjini na Segerea, Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara Prof. Abdalla Safari ataongoza timu katika majimbo ya Kisarawe na Temeke.

Makamu Mwenyekiti wa Chama (Zanzibar) Said Issa Mohamed ataongoza timu katika Jimbo la Ubungo huku Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji akiongozatimu katika majimbo ya Kibaha Vijijini na Ukonga.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Tanzania Bara, John Mnyikaataongoza timu katikamajimbo ya Bagamoyo na Mbagala huku Naibu Katibu Mkuu wa Chama Zanzibar akiongoza timu katika majimbo ya Mafia na Kawe.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ataongoza timu katika majimbo ya Chalinze na Kinondoni, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ataongoza timu katika majimbo ya Mkuranga na Kibamba.

Mjumbe wa Kamati Kuu Profesa Mwesiga Baregu ataongozatimu katikamajimbo ya Kibiti na Kigamboni huku Mjumbe wa Kamati Kuu Halima Mdee akiongoza timu kwenye majimbo ya Rufiji na Ilala.

Wajumbe wenginewa Kamati Kuu watakaokuwakatikaziarahiyo ni pamoja na; Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Arcado Ntagazwa, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Hashim Juma Issa, John Heche, Joseph Mbilinyi, na Boniface Jacob.

Imetolewa leo Jumatano, Machi 15, 2017 na;
Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
 
Safi sana chadema , hii ni muendelezo wa ile operesheni KATA FUNUA , wakati wao wanahangaika na individuals sisi tunasonga .

Hivi mkuu Makene , kama nimeguswa na nina vijihela kidogo nachangia vipi hiyo ziara ?
 
Back
Top Bottom