Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waharakisha shirika la mafuta Zanzibar

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
kificho.JPG


[h=1]
670.JPG
[/h]Posted on July 16, 2012 by zanzibaryetu
WAJUMBE wa baraza la wawakilishi wamepitisha makadirio ya matumizi ya wizara ya ardhi, makaazi maji na nishati ya mwaka wa 2012/2013 huku wakitaka uanzishwaji wa shirika la mafuta la Zanzibar ifikapo Januari mwakani. Wajumbe wengi hasa ambao wasiokuwa mawaziri (backbenchers) walionesha kutoridhika na majibu ya serikali kuhusu sababu za kutoendeleza utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika visiwa vya Zanzibar.
Huku wakitishia kuikwamisha bajeti ya wizara hiyo wajumbe hao walisema ni muda mrefu umepita bila ya dalili zozote za kuendeleza utafutaji wa mafuta na kuitaka serikali kuwa na msimamo usioyumba.
“Ni muda mrefu kila ahadi ndio hizo kwa hivyo tunasubiri utatuzi wa kero za muungano lakini wenzetu wanaendelea na mambo yao. Tunataka sheria ya kuanzisha shirika la mafuta ya Zanzibar ifikapo Januari mwakani bila ya hivyo tutaleta hoja binafsi ya kuazishwa shirika hilo” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa huku akiwataka wenzake wamuuonge mkono.
Akijibu hoja mbali mbali za wajumbe hao waziri wa wizara hiyo, Ramadhan Abdallah Shaaban alisema serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuondoa mafuta na gesi katika orodha ya mambo ya muungano lakini inashindwa kuleta mswada kutokana na kizingiti cha katiba zote mbili ya Zanzibar na ile ya muungano.
“Mheshimiwa Spika nimeapa kuheshimu na kulinda katiba zote mbili kwa hivyo siwezi kufanya haraka kuleta mswada barazani hadi hapo suala hili litakapotatuliwa na kwa bahati nzuri hoja hii ya mafuta ni miongoni mwa ajenda za baraza la mawaziri la muungano lijalo” alisema Shaaban.
Kutokana kutoridhika na majibu hayo wajumbe wakiwemo Makame Mshimba Mbarouk (CCM), Hamza Hassan Juma (CCM) Omar Ali Shehe (CUF), Hija Hassan Hija (CUF) na Mbarouk Wadi Mussa (CCM) wote waliitaka serikali kuachana na mwendo wa jongoo katika kushughulikia suala hilo.
Hali hiyo imemfanya makamo wa pili wa rais balosi Seif Ali Iddi ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali aktika baraza la wawakilishi kunyanyuka na kutoa ufafanuzi ili kuwapooza wajumbe.
“Mheshimiwa Spika serikali haijakaa kimya na tunashughulikia suala hili kwa juhudi zote kwa bahati nzuri rais wa jamhuri wa muungano na waziri mkuu wametoa matumaini na kukubaliana na hoja ya msingi kwa kusema inawezekana mafuta na gesi kuondoshwa katika orodha ya muungano. Naomba wajumbe wawe wavumilivu” aliahidi balozi Seif.
Backbenchers wanataka serikali iharakaishe kuleta mswada wa sheria wa kuanzishwa shirika la maendeleo la mafuta Zanzibar ili kutoa fursa kwa makampuni ya nje kuanza utafutaji na ushimbaji wa mafuta ili Zanzibar iondokane na changamoto ya uchumi.
Mafuta na gesi asilia imekuwa ni hoja nzito ndani ya baraza la wawakilishi tangu mwaka 2009 ambapo baraza lilipitisha azimio la kutaka rasilimali hizo kuondoshwa katika orodha ya mambo ya muungano kutokana na kutoridhika na serikali ya muungano katika rasilimali asilia.
Kwa mujibu wa katiba rasilimali asilia ikiwemo mafuta, gesi, dhahabu, almasi, fedha, tanzanite na makaa ya mawe vyote ni mambo ya muungano lakini tangu kuasisi kwa muungano mwaka 1964 zanzibar inalalamikia kutopata mgao wa rasilimali hizo.
MWISHO
Ukosefu wa mahakama za watoto
WAZIRI wa ustawi wa jamii maendeleo ya vijana wanawake na watoto Zanzibar, Zainab Omar Mohammed amesema wizara yake imechelewa kuanzisha mahakama maalumu ya watoto kutokana na ukosefu wa fedha.
Akijibu suali la msingi la mwakilishi wa jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub alisema taratibu za kuwashughulikia watoto walidhalilishwa ikiwemo kubakwa katika mahakama za kawaida.
Mwakilishi alitaka kujua sababu za msingi zzinazopelekea kukosekana kwa wataalmu wa kisheria na mahakama maalumu ya watoto wakati vitendo vya ubakaji vinaendelea.
“Mheshimiwa Naibu Spika sababu kubwa zinazopelekea kukosekana kwa wataalamu wa sheria katika wizara ni ufinyu wa bajeti wa ajira mpya serikalini” alisema Bi Zainab.
Hata hivyo alisema wizara yake inaendelea na juhudi za kutafuta fedha za kuanzisha mahakama maalumu ya watoto, na kwamba tayari wizara yake imeshaomba serikalini kukubaliwa kwa ajili ya angalau mwanasheria wa wizara kwa mwaka huu wa fedha.
Alisema pamoja na hali hiyo ya ukosefu wa mwanasheria kesi 10 kati ya 83 zilizoripotiwa wizarani kwake zinashughulikiwa katika mahakama ya kawaida.
Akitoa jibu la nyongeza waziri wa sheria na katiba Abubakar Khamis Bakari alisema kwa hivi sasa kesi za watoto zinasikilizwa katika vitengo maalumu na mahakimu wa wilaya ambao wamepewa jukumu hilo wakati serikali ikijiandaa kuanzisha mahakama maalumu za watoto.
MWISHO.
Magendo ya karafuu
JUMLA ya kilogramu 848 za karafuu zimekamatwa katika msimu wa huu uliomaliza wa mvuno ya karafuu zikiwa zinapelekwa nje ya nchi kwa njia ya magendo.
Hayo yameelezwa na naibu waziri wa wizara ya biashara, viwanda na masoko Thuwaiba Edington Kisasi wakati akijibu masuali kutoka kwa wajumbe waliotaka kujua karafuu zinazokamatwa zinapelekwa wapi.
Kisasi alisema katika msimu wa karafuu uliokwisha mwezi huu karafuu zote zilizokamatwa zilikuwa na thamani ya milioni 12.7 ambazo zilitaifishwa na mapato kugaiwa katika mafungu matatu kwa mujibu a sheria.
Mafungu hayo ni asilimia 50 ya mgao ni mkoa uliohusika na ukamataji, asilimia 20 inatolewa kwa aliyetoa taarifa za kimagendo na asilimia 30 ni mgao wa walioshiriki katika ukamataji wa karafuu hizo za magendo.
Naibu waziri huyo alisema karafuu hizo zilikamatwa katika mkoa wa kaskazini Pemba lakini kwa ujumla magenzo ya karafuu yalipungua sana katika msimu uliopita kutokana na ushirikiano mzuri wa wananchi.
Wajumbe wa baraza hilo Mohammed Haji Khalid (CUF) Subeit Khamis Faki (CUF) na Salim Abdallah Hamad (CUF) walitaka kujua katika ukamataji wa magendo ya karafuu, taratibu zinazofuatwa ili kudhibiti uhalifu nchini.
Katika msimu uliopita serikali ya Zanzibar ilifanikiwa kupata zaidi ya tani 4000 za karafuu na kuuza nje ambapo viongozi wa Zanzibar wanaeleza kutaka kuimarisha zao hilo ili kusaidia katika kuimarisha uchumi wake.
MWISHO
Barabara ya forodhani
ZANZIBAR imo katika matayarisho ya kujenga bandari mpya ya kisasa itakayokuwa na hadhi ya kipekee katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.
Hayo yameelezwa na naibu waziri wa miundombinu na mawasiliano Issa Haji Ussi alipokuwa akijibu swali la msingi la mwakilishi wa jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashm Ayoub aliyetaka kujua matayarisho ya kujenga bandari huru mpya.
Ussi alisema kauli ya serikali juu ya azma ya kujenga bandari mpya na ya kisasa yenye hadhi ipo pale pale na mradi huo utaanza katika kipindi kijacho.
Alisema bandari huru itakaojengwa inakusudia kutoa ushindani wa kibiashara na bandari nyeginezo ikiwemo ile ya Dar es salaam na Mombasa Kenya.
“Hakuna kitu kilichozuia isipokuwa suala la gharama za ujenzi na kampuni ya China ndio inayochelewesha kwa sababu tunataka kufikia makubaliano kabla ya kazi ya kuanza kwa ujenzi huo utakaoanzia na upembuzi yakinifu” alisema naibu waziri huyo bila ya kutaja kiwango cha fedha kilichotengwa.
Wakati huo huo huo serikali imekusudia kudhibiti wa uingiaji wa magari katika mji mkongwe ili kuhifadhi mji huo kutokana na kasi inayoendelea ya kuharibika kwa majengo ya mji huo wa kitalii.
Naibu wa wizara hiyo alisema njia za mji mkongwe zilifanywa kuwa ni nyembamba kutokana na kudhibiti uingiaji wa magari hasa makubwa.
“Mheshimiwa naibu spika baadhi ya njia zimefungwa katika mji mkongwe kutokana na kupunguza harakati za magari, magari yenye uziti usiozidi tani mbili ndio yanayoruhusiwa kuingia katika mji mkongwe” alisema.
Akijibu masuali kutoka kwa mwakilishi wa jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub na mwakilishi wa mji mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu, naibu waziri huyo alisema mji mkongwe kimaumbile sio mji wa magari na ushahidi wa hayo ni vichochoro vilivyomo katika mji huo.
“Sheria ya uhifadhi wa mji mkongwe zimekuja kulinda majengo pamoja na maeneo ya wazi yaliyomo katika hifadhi, kwa hivyo tunataka kuimarisha sheria hizo za uhifadhi ili kupunguza wingi wa magari kwa mji katika mkongwe” alisema Ussi.
Wawakilishi hao walionesha wasiwawasi wao juu ya kuongezeka kwa harakati za magari na maeneo ya wazi kuchukuliwa jambo ambalo linahatarisha uhifadhi wa mji mkongwe kwa mujibu wa shirika la maeneo ya elimu na sayansi (UNESCO).
Kuwepo kwa bandari isiyokuwa rasmi ya forodha mchanga pia ni miongoni mwa mambo ambayo yanaongeza shughuli nyingi zinazohatarisha uhifadhi wa mji mkongwe kutokana na magari makubwa kupitishwa katika bandari hiyo.
Hata hivyo naibu waziri ameahidi kuhakikisha kwamba bandari hiyo ambayo hutumika zaidi kwa kupakia magari makubwa kutoka Unguja kwenda Tanzania bara na Pemba inafungwa.
MWISHO
Huduma za uzazi bure
HUDUMA za bure kwa mama waja wazito zimeelezwa kuwa ni fursa itayopunguza vifo vya akina mama hao baada ya kuondoshwa ada ya huduma hiyo.
Mwakilishi wa jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub licha ya kupongeza hatua ya kuondosha ada ya uzazi iliyotangazwa hivi karibuni na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein alitaka huduma hiyo isambaze hadi vijijini.
“Jee wizara imejitayarisha vipi kuhakikisha kwamba akina mama wote wanaojifungua vijijini na mijini wanapata huduma za bure kama alivyoahiza rais? Alihoji mwakilishi huyo.
Aidha mwakilishi huyo alitaka kujua mpango wa wizara ya kuongeza madaktari wa kutosha wanawake ili kuondoa kilio cha akina mama kusaidia kujifungua na madaktari wa kiume.
Naibu waziri wa afya Dk Sirra Ubwa Mwamboya alisema baada ya agizo la rais wizara yake imekuwa ikichukua hatua mbali mbali za kununua madawa na vifaa na kusambaza maeneo yanayohusika.
Dk Sirra alisema shirika la maendeleo la Denmark (DANIDA) pia linasaidia kuhudumia vituo vya afya na hospitali za wilaya kutokana na mchango wa vifaa muhimu kwa ajili ya kuwaisaidia akina mama waja wazito.
Lakini Dk Sirra akizungumzia suala la kuongeza madaktari wanawake kuchukua fani ya utaalamu wa maradhi ya kike (gynecologist) alisema wanawake wengi hawapendi kusomea fani hiyo tofauti na wanaume ambapo wanasomea kwa wingi.
“Kwa hivi sasa katika hospitai zetu hakuna daktari hata mmoja wa kike mtaalamu wa maradhi ya kike kwa hivyo natoa wito tuwahimize watoto wetu wanawake wasome masomo ya sayansi na wachukue udaktari wa wanawake” alihimiza Dk Sirra.
Alisema kwa hivi sasa kwa habati mbaya kutokana na madaktari wanawake kutokuwa wengi ndio maana akina mama wana wazito wanapata huduma wanazojaaliwa kwa kuhudumiwa na wanaume na hawapati wanachokitaka.
MWISHO
Ucheleweshaji wa kesi
WIZARA ya Sheria na Katiba Zanzibar imetangaza kuendelea kupambana na tatizo la ucheleweshaji wa kesi katika mahakama ya Zanzibar na kuhakikisha matatizo ya wananchi katika usimamizi na ufuatiliaji wa haki zao yanapungua kwa kiasi kikubwa.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 waziri wa wizara hiyo, Abubakar Khamis Bakari pia alisema wizara yake imejipanga kushughulikia tatizo la ucheleweshaji wa vyeti vya kuzaliwa jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi wengi.
“Katika kuhakikisha kwamba kesi hazichelewi pamoja na upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa wizara imejipanga kukuza uratibu na usimamizi kwa kuwajengea uwezo watendaji ili waweze kumudu vyema kazi zao” alisema Bakari.
Alisema katika kipindi cha julai mwaka jana hadi machi mwaka huu jumla ya kesi 5,477 zilifunguliwa katika mahakama mbali mbali Unguja na Pemba ikiwa ni upungufu wa kesi 2,894 ukilinganisha na mwaka 2010 ambapo kesi 8,371 zilifunguliwa.
Waziri huyo akiomba wajumbe wajadili na kupitisha bajeti ya wizara yake alisema hali hiyo ya upungufu wa kesi inaonesha ufanisi zaidi katika masuala yanayohusu jinai pamoja na wizara yake kuimarisha ushirikiano na jeshi la polisi kuharakisha upelelezi.
“Kati ya kesi 5,477 zilizofunguliwa, kesi 1,308 ilikuwa ni za madai na kesi 4,0740 za jinai, ambapo kesi 2,604 sawa na asilimia 48 zimetolewa uamuzi katika kipindi hicho” alisema waziri.
Alisema wizara yake inafahamu vyema kwamba utendaji wa baadhi ya wafanyakazi wakiwemo makarani na mahakimu hauridhishi kutokana na rushwa hasa katika kesi za madawa ya kulevya, ubakaji na migogoro ya ardhi mambo ambayo hulalamikiwa sana na wananchi.
“Mheshimiwa naibu spika matatzo haya hata mimi yananikera sana na hivi sasa nimeshaanza kuyachukulia hatua. Zaidi ya mtazamo wetu sasa ni kuwa na kesi za vipindi (session cases) ili kuharakisha kesi hizi za madawa ya kulevya na ubakaji” aliwaambia wajumbe.
Waziri huyo alisema katika kuimarisha utendaji kazi katika mahakama jaji mkuu pamoja na watendaji wengine waliofanya ziara katika vyuo vya mafunzo (jela) ili kubaini matatizo yanayowakabili wafungwa na mahabusu yakiwemo masuala ya mrindikano, ucheleweshaji wa maamuzi na upatikanaji wa nakala za hukumu.
Waziri pia alisema wizara yake imo katika juhudi za kuimarisha majengo ya mahakama ili kuondokana na majengo chakavu pamoja na kutanua nafasi za kufanyia kazi.
Akizungumzia kuhusu usajili wa vizazi na vifo ikiwemo upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa waziri alisema mwaka jana jumla ya vizazi 36,123 vimesajiliwa wanaume wakiwa ni 20,711 na wanawake 15,412.
Kwa upande wa vifo vilivyosajiliwa ni 2,751 wanaume ni 1,688 na wanawake 1,063 wakati ndoa zilizosajiliwa ni 3,125 kupitia kwa masheikh na ndoa zilizosajiliwa kupitia mahakamani ni 125 na talaka 375, Unguja na Pemba.
 
Kwanza nikuharakisha kuvunja Muungano Fake na kupata nchi yetu ilokuwa huru, halafu ndio vilivyomo ndani ya nchi vitajilinda wenyewe.

Hivi sasa kuna uzaifu mkubwa wa tafauti za mitizamo ya wananchi wa Zanzibar na viongozi wa Smz ,wazanzibar Muungano hawautaki viongozi bado wana unafiki, sasa chakuchangaza yupi bosi wananchi au watumishi wa smz.
 
Kwanza nikuharakisha kuvunja Muungano Fake na kupata nchi yetu ilokuwa huru, halafu ndio vilivyomo ndani ya nchi vitajilinda wenyewe.

Hivi sasa kuna uzaifu mkubwa wa tafauti za mitizamo ya wananchi wa Zanzibar na viongozi wa Smz ,wazanzibar Muungano hawautaki viongozi bado wana unafiki, sasa chakuchangaza yupi bosi wananchi au watumishi wa smz.
Mbona kwenye mjadala wa katiba unaoendelea sehemu mbalimbali Zanzibar wananchi wengi wanaonyesha kuridhishwa na muungano uliopo,wewe unazungumzia wananchi wepi?
 
Mbona kwenye mjadala wa katiba unaoendelea sehemu mbalimbali Zanzibar wananchi wengi wanaonyesha kuridhishwa na muungano uliopo,wewe unazungumzia wananchi wepi?

Wengi ni wale ambao wameajiriwa kwenye serikali ya Muungano ,sasa usitegemee kama watasema hawataki muungano kwani watachukua miaka kulipwa mafao kama watalipwa.

Na uelewa kuwa kuna changa la macho hapa,kinachojadiliwa ni katiba ya Muungano wewe unaenda unasema unataka Muungano wa serikali tatu ,sijui moja wengine mbili ,hayo ni mambo tofauti. Hii ni hatari na tayari imeanza kushtukiwa .

Yakhe tunajadili Katiba ya Muungano ,hatujadili Muungano ,kwa Maana Muungano tayari upo ,sasa wewe unakwenda na tai yako unasema unataka serikali X ,hayo yanatiwa kapuni sawa na kura iliyoharibika.
 
Back
Top Bottom