GE2025 Wajumbe Kata ya Bonyokwa na Kinyerezi wabaki kulinda kura

GE2025 Wajumbe Kata ya Bonyokwa na Kinyerezi wabaki kulinda kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Wajumbe wa Kata za Bonyokwa na Kinyerezi zilizopo katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam wameamua kulala na wengine kuweka vijiwe nje ya kumbi walizopigia kura.

Kata za Jimbo la Segerea zina wajumbe zaidi ya 1,000 kwa kila kata, hivyo wengi wamesema kuwa huenda kazi ya kuhesabu kura ikachukua muda mrefu tofauti na matarajio.

Miongoni mwa wajumbe waliokutwa maeneo ya nje ya kumbi hizo leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 wamesema wamebaki maeneo hayo ili kulinda kura zao.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walionekana kutoka nje na kupanda bodaboda wakielekea majumbani na wengine kwenye mizunguko yao.

Mwenyekiti mstaafu wa kata ya Bonyokwa na mjumbe wa shina namba moja Bonyokwa Kisiwani, Mhidini Magimbi amesema wataendelea kusalia eneo hilo mpaka wahakikishe kura zinahesabiwa na mshindi anatangazwa.

“Upigaji wa kura utaratibu ulikuwa ni mnaitwa tawi kwa tawi unapiga kura na kutoka nje, hivyo uadilifu wa ndani hatujaujua bado,” amesema.

 
Back
Top Bottom