Wajue MADIKTETA 11 wenye vituko

Nadhani mkuu hukunisoma vema, utakubaliana nami kwamba madikteta wengi wamekuwa wakitumia rasilimali za nchi zao kujinufaisha, ilhali wakiacha watu wao katika lindi kubwa la umasikini. Tofauti ya Dikteta huyu na wengine ni kwamba pamoja na madhambi yake lakini sehemu kubwa ya rasilimali za nchi yake alizizitumia kuboresha maisha ya watu wake. Kumbuka maendeleo ni maendeleo ya watu na si Mabarabara ya hewani n.k. Udikteta wake kimsingi ulikuwa dhidi ya wapinzani wake na uadui wake ilikuwa dhidi ya mataifa ya magharibi. Hakukubali rasilimali za nchi yake kuporwa kwa kubadilishana na vyandarua. Na kwa kukufumbua macho ndugu yangu huo ndio udikteta wa Mugabe pia. Ni dikteta kwa sababu alirudisha ardhi kwa wananchi toka kwa wazungu waliomiliki 75% ya ardhi yote.
Kama kweli hawa jamaa wanapigania demokrasia ya kweli Kibaki na JK wasingekuwa madarakani (Wote EA tunajua ukweli huu).
Hila za magharbi siku zote zimekuwa ni devide and rule, walimwita Saddam anasaidia ugaidi, akaitwa dikteta akanyongwa na watu wake (vibaraka wa marekani), deal ilikuwa reserve ya mafuta. Leo kiko wapi? Siera Leone wameuwana kwa ajili ya Diamond, pesa ya mmarekani victim Charles Taylor. Congo mpaka leo wako vitani (mkono wa mmarekani), deal dhahabu. Na hata hapa JK asingekuwa mtu wao, wangetafuta vibaraka wengine wakawapatia silaha na fedha na tungeuwana tu. Tena hapa wana interest chungu nzima. Hatuyaoni sababu viongozi wetu na sisi wenyewe ni "YES SIR".
AM STANDING TO BE CORRECTED, COL. M. GADAFFI IS A HERO HE FOUGHT FOR HIS COUNTRY AND HE DIED IN HIS COUNTRY FIGHTING!
 

Mwengine ni Julius Kambarage Nyerere (Baba wa Taifa la Tanganyika)...
 
Dikteta anayewaletea maisha bora wananchi wake na mdemokrasia anayewasababishia wananchi wake maisha magumu, NI NANI KATI YAO ALIYE DIKTETA KAMILI?? Mimi nadhani udikteta ni mfumo tu wa kuingia madarakani kama ilivyo kwa demokrasia kwa wananchi kupiga kura zao.
 

12 Mh Slaa, Mgombea na Katibu mkuu wa CHADEMA

  • Atavunja Vyama vyote vya Upinzani akichaguliwa kuwa Raisi wa Tanzania.
  • Amepiga marufuku mgombea mwingine yeyete toka Chama chake kuchukua fomu ya kugombea Urais mpaka Afe
  • Haamini katika Demokrasia
 

Gadafi anautajiri uliofichwa seheme mbalimbali unaokadiriwa kufikia dola bilioni mia mbili ($ 200 bn) kwa mujibu wa the los angeles times. Oooohhhh yeah gadafi ni hero aliyekufa "akiipigania nchi yake".
 
Genghis Khan hamna rekodi zake? Alishindwa kuitawala India sababu aling'atwa na Mmbu hivyo aliichukia sana hiyo nchi na akawa anaikwepa
 

Mambo mazuri yalioorodheshwa kuwa Ghadafi alikuwa akiwafanyia RAIA WA Libya no sasa lakini haikuwa Libya yote,kuna taarifa kuwa alikuwa anafanya hayo kwa watu WA jiji WA Tripoli tu,miji mingine zilikuwa zinateketea kwa shida,ndo maana uasi ulianzia Benganzi na wala sio Tripoli
 
Mkuu tatizo watu wanatofautisha kati ya wajibu wa serekali na kuona kama fadhila. Kama uwezo upo serekali inapaswa kufanyia mema raia wake lakini lazima kuwe na uhuru wa kweli kwa hao raia.
Hivi uwajibu huo wa kutenda hayo alikuwa nao Gadaf pekee? Au ni viongozi wote? Hebu tupeni mfano wa kiongozi mwingine aliefanya kama yeye.

Hebu jaribu kutafakari,pato hilo lingekuwa kwetu Tanzania,viongozi wetu wangefanya kama alivyofanya Gadafi?
Au wangefanya ufisadi wa kutisha na kuishi kwenye ulimwengu wao wakipekee.!?

Jaribu kufikiria idadi ya faru iliyobaki kwenye mbuga zetu na tukio la faru John,bila shaka utakubali kuwa Gadafi pamoja na yoote hakuwasahau raia wake.
Aliwagawia japo kidogo keki ya taifa
 
Ukijiongeza kidogo tuu utaelewa kuwa,hilo ni neno la kisiasa kuonesha hatoipendelea familia yake bali atawatanguliza walibya
 
Ulipomtaja Gadaffi natamani ungekuwa karibu nikuzabe kofi la maana,hapo ndipo utagundua bado ukombozi unahitajika maana wengi mnashikiwa akili na wakoloni,Mungu amrehemu Gadaffi
 
Wapo wasomi wengi nchini....wengi wana "KASUMBA"....Wamekalilishwa (zaidi kutoka nyumba za KIROHO)
Na ni ngumu kwao KWELI YA LEO.....KUWEZA KUITOLEA USHUHUDA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…