Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Ndugu zangu ni vizuri kukumbushana, labda na kufahamishana juu ya mategemeo ambayo watanzania wote wanayo juu ya kizazi cha vijana kutokea miaka ya 80 hadi leo hii kwa taifa la Tanzania.
Kuna mambo ambayo ni ya kawaida sana ambayo kijana yoyote anategemewa kuyatekeleza. Jamii inamtegemea kijana wa kiume awe baba mzuri wa familia na kijana wa kike awe mama mzuri wa familia. Jamii inamtegemea kijana awe mstaarabu, mtanashati na mwenye busara. Mtu anayeshiriki shughuli za kijamii, anayefanya biashara kwa uaminifu na anayeheshimu wakubwa.
Ila kuna majukumu ambayo yanatofautisha kizazi kimoja na kingine.
Kwa mtazamo wangu Tanzania inamtegemea sana kizazi hiki katika kubadili kama sio kuimarisha historia yake.
Kijana anategemewa awe mkakamavu, shupavu, mzalendo anayeweza kuweka kifua mbele kulipigania taifa lake.
Kijana huyu anapaswa kutambua adui yake, adui anayemkwamisha kutekeleza majukumu ya kizazi chake; adui huyu ni mawazo mgando ya kuamini mamlaka za uongozi ziko sahihi na hazipaswi kuhojiwa hata kama dosari zinaonekana waziwazi.
Kijana anapaswa kupiga vita uoga na namna yoyote ile. Uoga ni ulemavu, ni homa inayomuingia mtu kwenye tumbo na kugandisha akili yake huku ikimuachia vipele vya baridi kwenye ngozi. Kijana anapaswa kusimamia usahihi wa mawazo yake hata ikiwa dhidi ya jeshi lenye silaha. Ujasiri na werevu wake unapaswa kumpa mbinu za kuruka vizuizi vilivyo mbele yake.
Kijana ana wajibu wa lazima wa kushiriki katika siasa kama mwanaharakati hai kwakuwa siasa ndio elimu ya haki.
Hapa kijana anapaswa kusikiliza, kuchambua na kuchangia. Kijana lazima alazimishe nafasi ya kushiriki katika harakati hizi hata kama mazingira ni magumu namna gani. Narudia; ujasiri na werevu wake vitampa mbinu.
Mkwamo wa kisiasa Zanzibar na ukimya wa vijana ni laana kwa taifa.
Ndugu zangu tukiacha hili likapita, tukakubali kutawaliwa na uoga na mawazo ya kibaguzi basi tutaenda kwenye makaburi yetu tukiwa na aibu kubwa itakayodumu vizazi na vizazi.
Unaweza kukosa yote katika maisha ila furahia kuwa kijana na kubali kuwajibika kwa taifa lako.
Asante!