Philipo D. Ruzige
JF-Expert Member
- Sep 25, 2015
- 9,429
- 27,123
Original post by Khalid Shekoloa
RSA TANGA REGION
*WAJIBU WA ASKARI AWAPO BARABARANI*
Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani
*Mamlaka ya kusimamisha gari lako*
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako
kama atakupa ishara ya kusimama.
Punguza mwendo kwa
usalama na utoke barabarani pia anaweza kukuuliza jina
na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama
Barabarani (RTA),s.78).
*Leseni ya kuendesha gari*
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako
ya kuendesha gari na pia anaweza kukataa fotokopi hata hivyo
unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya saa (72) siku tatu
kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.
Ili kuepuka matatizo, wakati wote tembea na leseni yako halisi kwenye
gari (RTA s.77).
*Hati ya usajili*
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama
yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima
liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu
vidogo kama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA
s.13).
*Leseni ya barabarani, na bima ya gari*
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni
halali ya barabarani na kibandiko cha bima kwenye kiwambo
cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).
*Kunyang’anywa*
Ofisa wa polisi *HANA* haki ya kuondoa vibandiko na
kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
*Mikanda ya kiti ya usalama*
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge
mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe
inatembea au imesimama) unatenda kosa kama
unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa
usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote
wafunge mikanda.
*Kuendesha baada ya kunywa pombe*
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na
huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe
(kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi
cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango
kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatia ya kosa (RTA
s.44, s.45, s.46).
*Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha*
Ingawa sheria *haikatazi* hili mahususi, ofisa wa polisi
anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “
kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).
*Mwendo kasi*
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni
pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo
yanaweza yasiwe na alama) ofisa wa polisi anaweza
kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata
hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA
s.51, s.73 (2)).
*Kustahili kuwepo barabarani*
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko
katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na
usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri.
Unaweza kutakiwa
kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi
wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).
Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua
kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.
KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA
UMEFANYA KOSA:
Mara nyingi utapewa uchaguzi wa
kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 30,000 kwa ofisa wa
polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka.
Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya *PF 101*, na
nyote wawili mtatia saini, kamwe usilipe faini bila ya kupata
nakala ya Fomu iliyotiwa saini.
Unaweza kwenda na ofisa
kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo.
Kama unakubali
kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza
jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA,
s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE UNAWEZA
KUTOA MALALAMIKO Muulize ofisa jina lake, cheo na
namba, na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi (unayo
haki ya kuuliza hilo ila kwa wengi huwa wakali sana na wakorofi)
Kisha peleka malalamiko ya
maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu ambaye
atachunguza na kujibu.
*Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu na wasikivu*
Tukutane kesho kwa somo lingine