Wahubiri,Mitume,na Wanasiasa mna deni kubwa kwa wanawake wa Tanzania

vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
420
Nianze Uzi huu kwakuwatakia heri na baraka wanawake wote ktk siku hii ya alhamis kuu,maana uwepo wao umesababisha maisha ya watu wengi kuwa mazuri kwa nafasi mbali mbali.

Nije kwenye hoja mujarabu ya kwanini wahubiri,mitume na wana siasa wanadeni kubwa kwa hawa mama zetu.Kwanza wanawake ndio wanaongoza kuhudhuria ktk nyumba za ibada za hao wahubiri na mitume kuliko wanaume na ni wafuasi wa kweli wa imani hiyo imepelekea mitume na wahubiri wengi kutumia mwanya huo,kujinufahiasha,na ikizingatiwa inapokuja suala la imani wanawake wanakuwa wepesi sana kuamini.

Pili kwa upande Wa wanasiasa wengi wameingia madarakani kutokana na kundi kubwa la wapiga kura wa uhakika(wanawake) rejea ushindi Wa ccm bara na ule wa mechi isiyokuwa na upinzani (Zanzibar) wanawake walijitoa haswa kufanikisha hill hivyo wanasiasa wenye mamlaka mnadeni kubwa kwa hawa ndg zetu ktk maeneo yafuatayo

1.Hakikisheni huduma za msingi za uzazi mnaziboresha ili kupunguza vifo vya wapiga kura wenu watiifu

2.Hakikisheni sheria kandamizi dhidi ya wanawake zinaondolewa

3.Huduma muhimi za kijamii,elimu,maji ni muhim zupatikane ili kuepusha akina mama kutembea umbali mrefu kufuata maji huku wakikumbana na changamoto nyingi

Kwa upande wa wahubiri,mitume na wale wote wanaofanya huduma za kiroho zinazowavutia wanawake wafanye yafuatayo

1.Epukeni kuwatoza michango mingi kanisani maana kufanya hivyo mnaharibu ndoa zao

2.Wainueni wahumini wenu kiuchumi badala ya kuwadidimiza

3.Waombeeni na wafundisheni kumjua mungu kiuhalisia hakika mtakuwa mmefanya jambo jema sana
 
Back
Top Bottom